Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro anawatangazia wananchi wote wa halmashauri ya Arusha kuwa, leo tarehe 15.02.2018, kutakuwa na Ugeni wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Kange Logola, pamoja na shughuli nyingine za kiusalama, atazungumza na wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara, utakaofanyika kwenye viwanja vya Stand ya Ngaramtoni kuanzia saa sita mchana.
Katika Mkutano huo Mheshimiwa Kange Lugola atatoa fursa ya kusikiliza kero za wananchi kuhusiana na masuala mbalimbali ya USALAMA.
Wananchi wote mnatakiwa kuhudhuria kwenye Mkutano huo muhimu bila kukosa.
Atakayesoma tangazo hili amuarifu na mwenzake.
*PAMOJA TUNATEKELEZA!*
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.