Wananchi wilayani Arumeru, wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya matarajio ya mvua za masika zinazotarajia kuanza mapema kuanzia mwezi Machi mpaka Mei, 2019.
Tahadhari hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Jerry Muro kupitia taarifa ya mwelekeo wa mvua inayotarajia kuanza mwezi ujao, kufuatia taarifa ya mwelekeo wa mvua za masika, liyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania - TRA.
Mheshimiwa Muro livha ya kuwatahadharisha wananchi kuhusu matarajio ya mvua hizo, amewataka watalamu wa halmashauri kujiandaa mapema kisekta, ili kujikinga na madhara ambayo mara nyingi hutokana na mvua hizo za masika.
Amesema kuwa, ni vema kujiandaa mapema, na kuitaka Idara ya Kilimo kuanza kuwaanda wakulima kwa ajili ya mapokezi ya mvua hizo, huku akisisitiza kuwaunganisha wakukima kupitia mitandao ya kilimo ndani na nje ya wilaya.
Amezitaka Mamlaka ya Barabara mijini na Vijijini -TARURA, kushirikiana na Idara ya Mazingira na usafishaji kupitia maeneo yote korofi kwa kusafisha na kuzibua mitaro pamoja na mifereji ambayo husababisha uharibifu wa barabara.
"Cha msingi ni kujiandaa mapema mtu wa kilimo asaidie wakulima kupitia mitandao yao , TARURA tujiandae na maeneo korofi na yale yenye kujaa maji tuangalie mitaro yetu mikubwa na tuhakikishe tunatumia Kamati za Mazingira na Usafishaji za kata kusafisha mapema " amesema mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha ameitaka Idara ya Afya kupitia Waganga Wakuu, kuchukua tahadhari ya kipindupindu mapema kwa kudhibiti viashiria hatari dhidi ya magonjwa ya milipuko.
Hata hivyo amewataka wananchi wote kujiandaa na ujio wa mvua hizo, pamoja na kuchukua tahadhari na madhara yanayoweza kujitokeza.
Bonyeza hapo chini kusoma taarifa ya TMA
MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA MACHI HADI MEI 2019.pdf
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.