• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ARUSHA DC VIJANA SSACCOS YAHUISHWA

Posted on: September 1st, 2019

Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana, Halmashauri ya Arusha imehuisha SACCOS ya vijana 'ARUSHA DC VIJANA SACCOS, kwa lengo la kuhamasisha na kuwajengea uwezo vijana wa kuweka na kukopa.


 SACCOS hiyo iliyokuwa imepoteza mwelekeo na kuwa kama imekufa kwa kipindi kirefu, imeweza kuhuishwa na kuanza upya kwa kuwakutanisha vijana wenye lengo la kuwa wajasiriamali, kwa ajili ya kuunganisha nguvu pamoja, kwa kuanza kununua hisa, kukopeshana wao kwa wao pamoja na nakukopesha vikundi vingine ili kuinuana kiuchumi.


Wakizungumza wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa SACCOS hiyo, kwenye ofisi ya vijana halmashauri, wanaSACCOS hao wamesema kuwa, wanatambua umuhimu wa kuunganisha nguvu ili kujengeana uwezo wa kupata mihitaji na kuanzishia  biashara kuelekea uchumi wa viwanda.


Nsesheye Nkota amethibitisha kuwa, SACCOS hiyo itarudisha matamani ya vijana wasio na ajira katika halmashauri ya Arusha na kuwapa fursa ya kupata mitaji, itakayowawezesha kujiajiri na kuondokana na changamoto ya vijana wengi kuwa uzururaji kwa kukosa ajira.


"SACCOS hii imeleta matumaini kwetu vijana, kutokana na wengi wetu, kukosa ajira na kushindwa kujiajiri kutokana na kukosa mitaji, hali inayosababusha vijana wengi kuwa wazururaji" amesema Nkota.

Aidha katika mkutano huo wa kwanza, umefanyika uchaguzi wa viongozi, na kumchagua, Evaline Zakayo kuwa mwenyekiti, makamu mwenyekiti ni Mihayo Zakaria  na  Hamidu Abubakary katibu ili kuiongoza SACCOS hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.


Akizungumza Mara baada kushinda nafasi ya mwenyekiti,  licha ya kuwashukuru wajumbe kwa kumchagua, Evaline ameahidi kufanya kazi kwa bidii,  ili kufikia malengo ya  SACCOS hiyo na kutimiza ndoto za vijana kuelekea uchumi wa viwanda.


Evaline amesema hii ni fursa nzuri kwakwe, ya kuhamasisha vijana wenzake,  kutumia fursa za kilimo na mifugo, zinazopatikana kwenye maeneo wanayoishi kwa kuziongezea thamani na kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini linalowakabili vijana wengi.

"Natambua dhamana niliyopewa , naamini kupitia nafasi hii nitapata fursa ya kukutana na vijana wengi, kazi yangu kubwa ni kuwahamasisha kubuni biashara zinazotokana na kilimo na ufugaji,  kwa kutumia mitaji midogo kuongeza thamani mazao hayo na kuanzisha viwanda vidogo.


Ameongeza kuwa, ukosefu wa ajira kwa vijana, umesababisha vijana wengi kukata tamaa na wengine kujikuta wakijiingiza kwenye vitendo viovu na kuwataka vijana kupambana ili kukabiliana hali ngumu ya maisha, bila kukata tamaa.


Sambamba na hayo ameitaka serikali kupita halmashauri zake nchini kuwejengea uwezo vijana wa kujitegemea pamoja na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali, kuweka na kukopo ili kuwasaidia kutambua njia sahihi za matumizi ya mikopo inayotolewa na  serikali.


Kwa upande wake Afisa vijana,  Halmashauri ya Arusha, Ahadi Mlai amesema malengo ya SACCOS hiyo ni kuwasaidia vijana kuweka akiba na kutumia akiba hizo kukopa, ili kuwainua kiuchumi na kuongeza wigo mpana wa kubuni na kutekeleza fursa za ajira zinazowazunguka.


Aidha, amewataka viongozi waliochaguliwa kuwa wabunifu, waaminifu na waadilifu katika kusimamia na kutekeleza majukumu ili kufikia malengo ya SACCOS hiyo.


ARUSHA DC VIJANA SACCOS imeanza na wanachama vijana 34, na inasimamiwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana kwa kushirikuana na Kitengo cha Ushirika, na kuhakikisha SACCOS hiyo inazaa matunda na vijana hao kufikia malengo.


Mwenyekiti wa ARUSHA DC VIJANA SACCOS, Evaline   Zakayo




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.