Halmashauri ya Arusha, imejipanga kutokomeza kwa kasi, utapiamlo mkali na ukondefu,kwa watoto walio chini ya miaka mitano, wanaokabiliwa na maradhi hayo,kwa kutoa tiba lishe, ndani ya halmashauri hiyo.
Mkakati huo umewekwa wazi na Afisa Lishe, halmashauri ya Arusha, Doto Milembe, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo, wahudumu wa vituo vya kutolea huduma za afya, ili kuweza kutoa tiba lishe hizo kwa watoto wenye, utapiamlo mkali na ukondefu.
Amesema kuwa, lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha watalam wa afya, wanawatambua na kutoa elimu ya lishe, kwa kina mama wajawazito, kuwatambua watoto wenye utapiamlo, kutoa chakula lishe pamoja na kuwafuatilia watoto kwenye ngazi ya familia na kuhakikisha familia zinapata lishe bora na kutokomeza kabisa utapiamlo na ukondefu kwa watoto wa chini ya miaka mitano.
"Takwimu za halmashauri ya Arusha, zinaonyesha bado asilimia 4 ya watoto wa chini ya miaka mitano, wanakabiliwa na Utapiamlo mkali katika na asilimia 7 wanakabiliwa na ukondefu, hivyo halmashauri imeweka mkakati wa kupambana na maradhi hayo na kuyatokomeza kabisa ifikapo 2025"amesema Doto.
Nao washiriki wa mafunzo hayo, wamekiri kupata uelewa mkubwa juu ya namna ya kuwatambua watoto wenye utapiamlo na kuwahudumia, na kuthibitisha uwepo wa watoto wenye utapiamlo katika maeneo yao, ya kutolea huduma za afya, huku changamoto kubwa ilikuwa ni tiba lishe, uwepo wa tiba lishe kwenye vituo, utasaidia kuwatibu na kutokomeza maradhi hayo.
Edna Maeda, muuguzi wa kituo cha Afya, Olkokola, amesema kuwa, mafunzo hayo yamemuwezesha kutofautisha mtoto mwenye utapiamlo na mtoto aliyepoteza maji mwilini kwa kuharisha, na zaidi namna ya kumpa huduma ya kwanza pamoja na kufuatilia matibabu yake ikiwemo chakula lishe.
Hata hivyo ameitaka jamii, kuzingatia ulaji wa chakula bora kwa watoto, chakula chenye kuzingatia makundi yote virutubisho vya lishe, jambo ambalo litajenga afya ya mtoto na kumuwezesha kukua vizuri kimwili, kiakili na kisaikolojia.
Ni vema kuhakikisha watoto wanapata lishe bora, kwa kuwa ukosefu wa lishe bora unasababisha utapiamlo na ukondefu na kumsababishia mtoto udumavu wa mwili na akili hatimaye, kuwa na taifa lenye watu wasio na afya bora, taifa ambalo litakosa nguvu kazi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.