Na. Elinipa Lupembe
Mkuu wa wilaya ya Monduli , mheshimiwa Idd Kimanta amehitimisha kazi ya kukaimu ukuu wa wilaya ya Arumeru jana, kwa kumtambulisha na kumka mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru.
Mheshimiwa Kimanta amemtambulisha mkuu wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro kwa watumishi wa wilaya hiyo yenye halmashauri mbili za Meru na Arusha.
Akizungumza wakati wa utambulisho huo, Mheshimiwa Kimanta ameanza kwa kumpongeza Jerry Muro kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru, na kumtaka kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu kama Rais alivyomuamini.
Mhe. Kimanta amefafanua kuwa, hana mashaka na uteuzi wa mheshimiwa rais kwa kuwa kila mkuu wa wilaya, anayemteua anauzoefu na kazi ya kuwahudumia wananchi.
"Kwa taaluma ya Jerry Muro, sina mashaka na uchapa kazi wake, na uwezo wake wa kuwahudumia wananchi wanyonge, hivyo mheshimiwa rais hakubahatisha kumteua" amesema mheshimiwa Kimanta.
Hata hivyo amewataka watumishi wa halmashauri ya Arusha, kumpa ushirikiano kama waliompa yeye katika kipindi chote alichofanya kazi katika halmashauri hiyo.
Mheshimiwa Kimanta amekiri, kuridhishwa na uwezo wa watumishi wa halmashauri ya Arusha na hakusita kuwapongeza watumishi hao mbele ya mkuu huyo mpya wa wilaya ya Arumeru.
" Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Arumeru, ninakukabidhi watumishi hawa, wakiwa weupe kama kitambaa, wakiwa wenye afya njema, wenye nyuso za bashasha na uwezo mkubwa wa kufanyakazi kwa weledi huku wakitekeleza Ilani ya Chama Tawala, chama cha Mapinduzi CCM" amesema mheshimiwa Kimanta.
Ameongeza kuwa, kwa kipindi kifupi alichofanyakazi wilaya ya Arumeru, amekiri kuona utendaji uliotukuka wa watumishi wa halmashauri ya Arusha wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Wilson Mahera, watumishi waliojikita zaidi kwenye kazi za kuwahudumia wananchi na si kwenye migogoro na ugomvi baina ya watumishi wenyewe.
Amekiri kuwa, watumishi wanafanyakazi wakiwa na amani ya kazi, kwa kuwa hajawahi kupokea lalamiko la mtumishi yoyote, akimlalamikia mtumishi mwenzake, jambo lililomuwezesha kujikita kwenye kufanyakazi zaidi na sio kusuluhisha kesi za ugomvi baina ya watumishi, na kukiri kuwa, hali hiyo ni tofauti sana na maeneo mengine aliyowahi kufanyakazi.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Idd Kimanta amekaimu kuitimikia wilaya ya Arumeru kwa takribani miezi nane sasa tangu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, mheshimiwa Pastory Mnyeti mapema mwishoni mwa mwaka 2017.
Licha ya ukubwa wa wilaya ya Arumeru kwa kuwa, na halmashauri mbili ya Arusha na Meru, amefanikiwa kusimamia vema na kwa weledi mkubwa licha ya kuzitumikia halmashauri tatu kwa wakati mmoja, kwa takribani miezi nane.
Watumishi wa halmashauri ya Arusha, wamempongeza mkuu huyo wa wilaya ya Monduli na kuthibitisha kuwa wamefanikiwa, kujifunza mambo mengi kutokana na hekima na busara za mzee Kimanta.
Wamesema kuwa uzoefu, busara na hekima za mkuu wa wilaya Kimanta, ni hazina kwa watumishi wa halmashauri ya Arusha na kuahidi kutumia katika kuwatumikia wananchi.
Naye Afisa Mipango, halmashauri ya Arusha, Anastanzia Tutuba amesema kuwa amejifunza, unyenyekevu, kujishusha kwa mtu yoyote bila kujali hadhi yake pamoja na kutumia muda usikiliza zaidi.
" Mzee Kimanta ni kiongozi mbobezi mwenye tofauti, licha ya kuwa na umri mkubwa na cheo kikubwa, lakini ni bado mnyenyekevu, anayejishusha, mwenye kusikiliza kabla ya kufanya maamuzi, kifupi ni kiongozi aliyetukuka" amesema Afisa Mipango huyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.