Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Jerry Muro, leo amefungua mkutano wa wabobezi wa utafiti katika ukanda wa Africa Mashariki 'The Eastern Africa Research and Innovation Management Association, Tanzania Chapter" uliofanyika kwenye.
Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, Mkuu wa Wilaya huyo, amewapongeza Watafiti kwa Ubunifu wa kuwa na Jukwaa la pamoja linalowakutanisha na kuwapa fursa ya kujadili kwa masuala mbalimbali yanayohusu tafiti wanazozifanya.
Ameongeza kuwa kukaa pamoja kunawezesha kupeana uzoefu na changamoto zinazowakabili wakati wa kufanya tafiti kulingana na maeneo yenu pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi wa jumuia ya Afrika ya Mashariki.
Aidha mheshimiwa Muro amewaeleza watafiti hao, kuwa Serikali ya Tanzania inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na watafiti nchini, hivyo kuwezesha taasisi za kitafiti na za Elimu ya juu katika kufanya tafiti mbalimbali nchini.
Hata hivyo ameeleza kuwa, serikali inasubiri kupata mrejesho juu ya changamoto zote, zitakazo bainishwa na wataalam hao na kujipanga kutoa ushirikiano stahiki katika kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Mheshimiwa Muro amemaliza kwa kuipongeza Taasisi ya Sayansi na Technolojia ya chuo kikuu cha kimataifa cha Nelson Mandela, kwa kuwa mfano mzuri katika kufanya tafiti, zinazogusa maisha ya watu na viwanda na kusema kuwa kazi kubwa iliyobakia ni kushirikiana katika kuzifikisha kwa jamii na viwanda.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.