Na. Elinipa Lupembe
Watumishi halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano bila kubaguana kwa vyeo wala nafasi walizonazo, ili kufikia malengo ya halmashauri yaliyoaanishwa kwenye mpango mkakati wa halmashauri hiyo, malengi yaliyojikita zaidi katika kuwatumikia wananchi.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, katika kikao kazi cha kawaida, kinachowakutanisha watumishi wote wa makao makuu ya halmshauri hiyo, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi Mahera, amesema kuwa kikao hicho kina lengo la kukumbusha watumishi haki na wajibu wao katika kufanya kazi za utumishi wa umma, kazi zilizojikita zaidi katika kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya serikali.
Amesema kuwa kila mtumishi ana haki sawa na anatakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku, kufanya kazi kwa weledi na kutumia taaluma yake aliayosomea kwa kushirikiana na watumishi wenzake ili kufikia malengo ya serikali.
Aidha amewataka watumishi hao kukaa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kuweka wazi kero walizo nazo ili ziweze kutatuliwa kwa wakati na menejimenti, badala ya kusubiri mpaka mambo yaharibike ndipo kuaza kulalamika.
Hata hivyo Dkt. Mahera amesisitiza kuboreshwa kwa dawati la malalamiko na kero katika halmshauri hiyo na kusisitiza kuwa malalamiko yote kushughulikiwa na idara husika kwa usimamizi wake, huku akiwataka watumishi noa pia kutumia dawati hilo kufikisha malalamiko yao ili yaweze kutatuliwa kwa wakati na kutambua kuwa dawati hilo si la wananchi peke yao.
“Dawati la malalamiko si la wananchi peke yao, hata ninyi watumishi linawahusu, unapopata tatizo lililoshindikana ndani ya idara au kitengo chako, wasilisha kwenye dawati hilo, ndio sehemu sahihi na litashughulikiwa kwa wakati, badala ya kulalamika huko jambo ambalo linaeneza chuki baina yetu” amesema Mkurugenzi huyo.
Naye Mkuu wa Idara ya Utumishi, halmashauri ya Arusha Hamis Mpume, amewaahidi watumishi hao kuendelea kusimamia haki zao, wajibu na usawa, na kuwakumbusha watumishi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ikiwa ni apamoja na kutekeleza wajibu wao na kuahidi kuwachukulia hatua watakaokwenda kinyume.
“Nina imani kila mtumishi anafahamu vizuri majukumu yake, niwatake kila mmoja wenu kuyatekeleza kwa ufanisi, mimi kama msimamizi wenu, nitatenda haki, sitamuonea mtu ila sitasita kumchukulia hatua stahiki yule asiotekeleza majukumu yake" amesema Mpume
Ameongeza kuwa, kuna haja ya kukutana na watumishi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi pamoja na kufanyika vikao vya idara na vitengo kila mwezi ili kushughulikia matatizo ya watumishi kwa wakati.
Hata hivyo watumishi hao, wameahaidi kutekeleza majukumu yao kama walivyosaini kwenye mikataba yao ya utumishi wa Umma na kumuomba mkurugenzi wao, kuwapa motisha katika utekel;ezaji wa majukumu yao, motisha ambayo huwaongezea ari ya kufanya kazi.
Simon Mwanjwangwa ambaye na Mhasibu wa halmashauri hiyo, licha ya kumshukuru Mkurugenzi huyo kwa kukaa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili amemuomba mkurugenzi huyo kutoa motisha chanya kwa watumishi pale wanapofanya kazi, jambo ambalo linawaongezea ari ya kufanya kazi pamoja na kupenda kazi yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.