Na. Elinipa Lupembe.
Jamii imetakiwa kuvunja ukimya na kuachana na mila potofu, za kudhani kumfundisha watoto masuala ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango ni kumfanya aanze kujiingiza kwenye mahusiano ya kingono mapema.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Afisa Mipango, Anastazia Tutuba, wakati akifungua kikao kazi cha siku moja kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha, kilichojumuisha wadau mtambuka wa afya ya uzai kwa vijana, amesema kuwa usiri miongoni mwa jamii, unasababisha watoto wengi kujiingiza kwenye mahusiano ya kingono katika umri mdogo kujikuta wakipata mimba za utotoni na ndoa za utotoni,
Ameitaka jamii hasa wazazi kuvunja ukimya na kuanza kuzungumza na watoto wao, juu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpamgo, kwa kuzingatia mabadiliko yao ya kimwili na kiakili yanayojitokeza wakati wa kukua kwa via vya uzazi, jambo litakalo wawezesha kukabiliana na mihemko ya mwili yanayotokana na mabadiliko hayo.
Vijana wengi wamejikuta wakishauriana wao kwa wao, huku wakipeana taarifa zisizo sahihi na kijiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na kuanza kujamiiana katika umri mdogo bila kufahamu madhara ya matokeo ya vitendo hivyo na kusababisha mimba zisizotarajiwa na ndoa za utotoni, huku vijana hao wakikatiza masomo na kushindwa kufikia malengo yao ya kimaisha.
Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yameweka mipango mingi ya maendeleo kwa jamii na taifa, wazazi na jamii isipokua makini, itakipoteza kizazi hiki na kushindwa kuendeleza mipango mizuri iinayoandaliwa na serikali sasa.
" Tuungane kuwafundisha vijana wetu masuala ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana, ili kuwa na kizazi chenye kujitambua na kutambua majukumu yao binafsi na ya taifa na si kuwa na vijana wenye msongo wa mawazo kutokana na kujeruhiwa na mahusino, yanayokatiza ndoto zao" amesema Tutuba
Hata hivyo, mratibu wa mradi shirika la JHIPEIGO, Arusha, Waziri Njau, amefafanua kuwa suala la afya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana ni jukumu la kila mtu, kuwa karibu na watoto, kuzungumza nao na kuwaelekeza kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kukutana na watalamu wa afya kwa ushauri nasaha, kutasaidia vijana kufikia ndoto zao.
Aidha amewataka walimu wa afya shuleni, licha ya kuwafundisha masomo mengine wapate nafasi ya kuanzisha klabu za afya, ili kuwajengea vijana uwezo wa kujitambua na kutambua afya ya uzazi inayoendana na mabadiliko yao kimwili, kiakili na kisaikolojia sambamba na jinsi ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko hayo.
Naye Afisa Vijana halmashauri ya Arusha, Ahadi Mlai amethibitisha kuwa, uelewa mdogo wa jamii juu ya afya ya uzazi kwa vijana, imekua ni changamoto inayokatiza ndoto za vijana wengi na kuitaka jamii kushirikiana kuwaelimisha watoto juu ya afya ya uzazi, na kuwasihi vijana kufika kwenye vituo vya afya kupata taarifa sahihi za afya ya uzazi kupitia Huduma Rafiki kwa Vijana zinazotolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya
Amesema kuwa kikao kazi hicho kimewakutanisha wadau wa afya ngazi ya halmashauri, maafisa watendaji wa kata, walimu wa afya shuleni, viongozi wa dini na jamii, lengo likiwa kuwa na uelewa wa pamoja juu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana, na wao kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa huduma hiyo kwa vijana.
Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO Tanzania, wanatekeleza mradi wa Tupange pamoja na Huduma Rafikoi kwa vijana, mradi unaofadhiliwa na Bill &Melinda Geti wa nchini Marekani.
Awali jumla ya vituo vya afya 15 vya halmashauri ya Arusha,vinatoa huduma Rafiki kwa Vijana, shime vijana tusione aibu, tukapate huduma ya afya ya uzazi, huduma zinatolewa bure na kwa usiri.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.