Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi na wafanyabiasha wote kuwa, kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni
Kuanzia tarehe 27.07.2018, Mnada wa Ngaramtoni unahamishiwa rasmi katika kata ya Olkokola eneo la Ilkurot.
Hivyo wafanyabiashara wote mnatakiwa kuhama na kwenda kufanyabiashara zenu katika mnada wa Ilkurot.
Mwananchi au Mfanyabiashara yoyote atayekaidi na kuonekana kuendelea kufanyabiashara katika mnada wa Ngaramtoni atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuitafishiwa mali zake atakazokuwa ameleta kwenye mnada.
Uongozi wa Halmashauri unaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi wote ili kuepuka usumbufu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.