• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TASAF KUOKOA WASICHANA NA NDOA ZA UTOTONI

Posted on: August 29th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF wameanza ujenzi wa mabweni, mawili ya wasichana shule ya sekondari mabweni Oldonyowas, kuokoa wasichana, kuondoka na ndoa za utotoni kwa kujenga mabweni

Wakizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa mabweni, wasichana wa shule hiyo, wamesema kuwa, uwepo wa mabweni utawasaidia wasichana wengi wa jamii ya wafugaji kuondokana na changamo ya ndoa za utotoni, zinazowakabili kutokana na mila na desturi za jamii hiyo.

Wamesema kuwa, wasicha wengi wa jamii ya wafugaji, wamekosa nafasi ya kuendelea na masomo na kukatisha ndoto zao, kutokana na mila na desturi zinazowasababisha, kuacha masomo na kuolewa na wengine kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo kutokana na kazi nyingi wanazofanya mara baada ya kutoka shuleni.

Malkia Losiyeku, mwanafunzi wa kidato cha kwanza, shule ya sekondari Oldonyowas, amethibiyisha kuwa, uwepo wa mabweni ya wasichana, utawaepesha na mambo mengi ya mila na desturi yanayoendelea nyumbani, ikiwemo kuachishwa masomo na  kuozeshwa katika umri mdogo.

Amesema kuwa anaamini, wasicha wakiwa bweni, watakuwa chini ya usimamizi salama wa walimu, usimamizi ambao utawafanya wazazi kuogopa kuwaondoa watoto na kwenda kuwaozesha kwa kuhofia watoto hao wako chini ya serikali.

Heavenligh Geophray amesema kuwa, uwepo wa mabweni ya wasichana, utawezesha ufaulu kwa kuwa wasichana wengi hukosa muda wa kujisomea nyumbani kutokana na wasichana kutumia muda mwingi kufanyakazi wanazopangiwa kufanya kila siku jioni, mara watokapo shuleni.

"Ukirudi nyumbani jioni, unatakiwa kwenda kuchota maji, kutafuta kuni, kupika, ukimaliza kazi hizo unakuwa tayari umechoka, huwezi hata kusoma tena, na asubuhi unatakiwa kuamka alfajiri kuwa shule, unakwenda shule umechoka na kurudi umechoka"amesema Heavenlight.

Ameongeza kuwa, wanafunzi wengine wanaishi mbali sana na shule, wanapita kwenye mapori na makorongo, mazingira ambayo ni hatarishi kwa wasichana, kuweza kufanyiwa vitendo vya ukatili, lakini uwepo wa mabweni, utasaidia kuepusha madhara ambayo yanaweza kumpata msichana njiani.

Hata hiyo mkuu wa shule ya Oldonyowas, mwalimu Richard Mugabuso, amethibitisha kuwa, ujenzi wa mabweni hayo ni muhimu kwa wasichana ambao wanachangamoto nyingi nyumbani na shuleni, hivyo wepo wa bweni, utawezesha wasichana kupata muda wa kujisomea, kuongeza ufaulu pamoja na kupandisha kiwango cha taaluma shuleni hapo.

Ana Lukas, mzazi mwenye mtoto wakike shuleni hapo, ameishukuru serikali kupitia TASAF kwa mradi huo wa mabweni, na kusema kuwa wasichana kukaa shuleni kutaleta amani hata kwa wazazi, kwani mtoto akienda shule, mzazi hukosa amani na kuwaza pengine atakutana na majaribu gani njiani.

Ujenzi wa mabweni mawili ya wasichana, shule ya sekondari Oldonyowas, uko kwenye hatua za awali na unatekelezwa na serikali kupitia miradi ya uboreshaji miundombinu, miradi inayotekelezwa na TASAF awamu ya III, kwa gharama ya shilingi milioni 144.7, mabweni  yanayotegemea kulaza wasichana 96, ikiwa wanafunzi 46 kwa kila bweni.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.