Na. Elinipa Lupembe
Jumla ya watoto elfu 83 wa kuanzia miaka 5 hadi 14, ndani ya halmashauri ya Arusha, wanategemea kupatiwa dawa za kinga tiba ya ugonjwa wa Kichocho na minyoo ya tumbo, magonjwa yanayofahamika kama magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele 'Neglected Tropical Disease (NTD)'.
Zoezi hilo la siku mbili, limeanza leo na linategemea kukamilika kesho, katika maeneo yote ya halmashauri hiyo, huku dawa hizo zikitolewa kwenye vituo 139, vilivyoko kwenye shule za msingi za serikali na zile za binafsi.
Akizungumza na mwandishi wetu Kaim Mganga Mkuu, halmashauri ya Arusha, Dkt. Peter Mboya, amesema kuwa zoezi limeanza vizuri, vituo vyote 139 vinafanyakazi huku watoto, wakiendelea kupatiwa dawa hizo za kinga tiba.
Amesema kuwa zoezi hilo ni la kitaifa, Serikali inatoa kinga tiba hiyo bure, kutokana na ongezeko la tatizo la magonjwa ya kichocho na minyoo kwa watoto ambayo husababisha upungufu wa damu, utumbo kutoboka na hata kifo.
Ameendelea kueleza kuwa, ugonjwa wa kichocho nao ni tatizo kubwa kwa watoto na usipopata tiba kwa haraka, husabisha madhara na wakati mwingine vifo, hivyo ni vema wazazi kuchukua tahadhari kwa kuwapa watoto dawa hizo pindi serikali inapoendesha zoezi la kuwapatia watoto dawa za kinga tiba.
Aidha amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao, wanapata kinga tiba hizo muhimu, ambazo hut kwa afya za watoto wao, na kuwaondoa hofu, wale wanaodhani dawa hizo zina madhara kwa watoto.
Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi, ametembelea baadhi ya vituo na kushuhudia zoezi la kutoa dawa hizo, likiendelea vizuri huku walimu na wanafunzi wakiwa ushirikiano wa hali ya juu.
*Pichani watoto wa shule ya Msingi Naurei kata ya Kiutu, wakimeza dawa wakati wa zoezi la kutoa kinga tiba hizo* .
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.