Na. Elinipa Lupembe.
Vyuo vya elimu ya Juu na Mafunzo ya Ufundi stadi, vimeshauriwa kuangalia namna ya kuandaa mpango mkakati, wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma kwa kuwaongezea ujuzi na maarifa, ili waweze kwenda na wakati na kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia yanayoikabili dunia sasa sambamba na kufanikisha adhma ya Serikali ya kuutumikia Umma wa watanzania kwa weledi.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha,Alvera Ndabagoye, wakati akifungua warsha ya siku moja, iliyotolewa na Chuo cha Uhasibu Arusha, kwa wakuu wa shule na walimu wa fedha wa shule za sekondari za Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha, mafunzo yaliyohusisha Saikolojia ya Uongozi na usimamizi wa fedha za Umma, yaliyotolewa jana chuoni hapo.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa, mafunzo kazini ni nyenzo kubwa kwa watumishi wa umma, nyenzo ambayo huongeza tija na ufanisi kazini pamoja na utendaji kazi unaoendana na wakati, kutokana na mabadiliko ya kila siku ya kiteknolojia.
Licha ya kuwa watumishi wameajiriwa kutokana taaluma zao lakini bado kuna umuhimu wa watumishi kupata mafunzo ya mara kwa mara wawapo kazini, mafunzo yatakayowezesha kuongeza weledi na kuvitaka vyuo kuandaa mkakati wa kutoa mafunzo kwa watumishi wanaovizunguka vyuo hivyo kwa gharama nafuu.
Serikali inashindwa kumudu kuwapeleka watumishi kwenye mafunzo, kutokana na gharama kubwa zinazopangwa na vyuo, na kuwataka viongozi wa vyuo kuangalia namna ya kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma kwa gharama nafuu.
"Unakuta chuo kinaandaa mafunzo kwa ajili ya watumishi wa kada flani, gharama ya mtu mmoja laki mbili wakati mwingine mpaka laki tano kwa wiki moja, halmashauri ina watumishi takribani elfu nne, ni vigumu sana kumudu kuwapeleka watumishi kwenye mafunzo hayo kutokana na gharama hizo" amesema Mkurugenzi Alvera
Mkurugenzi Alvera, licha ya kuushukuru uongozi wa chuo cha Uhasibu Arusha, kwa kuandaa mafunzo hayo, amewataka walimu kutumia ujuzi huo kwa manufaa ya umma na kuhakikisha fedha za umma zinatumika vizuri kulingana na kanuni, sheria na taratibu za matumizi ya fedha za Umma.
Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano kila mwezi inatoa fedha za elimu bila malipo, kiasi cha shilingi Bilioni 23.9 kwa nchi nzima huku halmashauri ya Arusha ikipokea takribani shilingi milioni 104.4 kwa mwezi, fedha ambazo zinakwenda kwenye akaunti za shule moja kwa moja, shule ambazo hazina wahasibu, hivyo mafunzo haya yatasaidia usimamizi wa mapato na matumizi sahihi ya fedha hizo.
Naye Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Profesa Aliamani Sedoyeki, amefafanua kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakuu wa shule na walimu wa fedha namna bora ya usimamizi wa fedha za Umma, unaozingatia weledi, kanuni, sheria na taratibu za matumizi ya fedha za Umma.
Ameongeza kuwa, kupitia rasilimali zilizopo chuonin hopo, chuo kimeaandaa mkakati wa kutoa mafunzo ya muda mfupi walimu wakuu na walimu wa fedha, katika usimamizi wa fedha za Umma, fedha ambazo Serikali inazipeleka moja kwa moja kwenye akaunti za shule pamoja na namna bora ya kutumia 'forced akaunti' kwenye utekelezaji wa miradi ya shule, lengo kuu ikiwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.
"Kumekuwa na changamoto kubwa ya matumizi ya fedha, kutokana na shule nyingi za serikali kutokuwa na wahasibu, jambo linalosababisha utunzaji wa kumbukumbu za fedha kuwa wa kusuasua, hata hivyo mafunzo haya yataleta tija na ufanisi kwenye usimamizi thabiti wa fedha za umma" Amesema Mkuu huyo wa chuo.
Hata hivyo wakuu hao wa shule hao, wameamathibitisha kuwa mafunzo hayo, yanatija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi za shule, kwa kuwa kitaaluma wengi wao si watalamu wa mambo ya fedha huku vyeo vyao vikiwa vimekasimiwa jukumu la usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za shule,
Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Oldonyowas, mwalimu Richard Migabuso, amekiri kuwa mafunzo hayo yatawaongezea maarifa ya usimamizi wa fedha za umma hasa kwenye kipengele cha matumizi ya firced akaunti pamoja na suala zima la ulinganifu wa hesabu 'banking reconciliation'.
Awali mafunzo hayo ya siku moja, yamehusisha takribani shule 50 za sekindari za mkoa wa Arusha, kutoka halmashauri mbili za Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, akizungumza na wakuu wa shule za sekondari za Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha, wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma, kwenye moja ya kumbi la midahalo chuo cha Uhasibu Arusha.
Mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Eliamani...... akizungumza na wakuu wa shule za sekondari za Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha, wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma, kwenye moja ya kumbi la midahalo chuoni hapo.
Afisa Elimu Sekondari, Halmashauri ya Arusha, mwalimu Medard Lupenza, akizungumza na wakuu wa shule za sekondari za Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha, wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma, kwenye moja ya kumbi la midahalo chuoni hapo.
Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari za Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha, wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa, wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma, kwenye moja ya kumbi la midahalo chuo cha Uhasibu Arusha.
Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari za Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha, wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa, wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma, kwenye moja ya kumbi la midahalo chuo cha Uhasibu Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.