Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, halmashauri ya Arusha wamepitia na kukagua jumla ya miradi 12, yenye thamani ya takribani bilion 3.5, miradi iliyolenga sekta ya Elimu, Afya,Maji, miradi ya serikali kupitia mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF pamoja na miradi iliyotekelezwa kwa nguvu za wananchi.
Ziara hiyo ya siku mbili iliyofanyika wiki iliyopita, imehusisha kata za Oldonyowas, Mwandet, Olturumet, Olmotony, Mlangarini, Nduruma, Bwawani, Oljoro na Kisongo, ikiwa na lengo la kukagua shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili cha kuanzia mwezi Okoba mpaka Desemba 2018.
Katika ziara hiyo wajumbe hao wa kamati ya fedha, wameridhishwa na utelekezaji wa miradi hiyo ya maendeleo kwa asilimia kubwa licha ya changamoto nyingi zinayojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maji, miradi iliyochukua muda mrefu kukamilika.
Wajumbe hao pia wamepongeza juhudi kubwa zinzofanywa na wananchi wa kata za Mwandeti kijiji cha Losikito na Kata ya Oldonyowas kwa kujitoa kwa hali na mali kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule katika maeneo yao na kuwataka wananchi wote kuiga mfano huo kwa maendeleo yao na vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, mheshimiwa Noah Lembris, amesema kuwa, asilimia kubwa ya miradi inayotekelezwa ndani ya halmashauri, inaridhisha kwa kigezo cha uhalisia wa mradi na thamani fedha yaani 'value for money' huku akiwapongeza wananchi kwa kujitoa kwa hali na mali kutekeleza miradi mwanzo mpaka kukamilika katika maeneo yao.
"Inatia moyo kuona wananchi wanajenga miundombinu ya shule mpaka kukamilika, wanachangishangishana mpaka shililingi milioni 300, haya ndio maendeleo tunayopaswa kujifunza wananchi wote Tanzania" amesema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo Kamati hiyo imewataka wananchi kuendelea kujitoa na kuthamini miradi iliyo katika maeneo yao na kuwataka kuitunza na kuijali kwa kuwa ni mali yao, huku serikali ikiwa ni wasimamizi.
Awali miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Losinoni Juu, shule ya sekondari Oldonyowas kata ya Oldonyowas, shule ya sekondari Losikito, ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Mwandeti, ujenzi wa wodi ya uzazi hospitali ya Olturumet, ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Olmotony Forest.
Ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kiseriani, umaliziaji wa kituo cha Afya Manyire, ujenzi na upanuzi wa kituo cha Afya Mbuyuni kata ya Oljoro pamoja na miradi ya maji ya Bwawani na Loovilukuny kata ya Kisongo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.