Na. Elinipa Lupembe.
Wakuu wa shule nane za sekondari na msingi, halmashauri ya Arusha, waliopokea fedha zilizotolewa na serikali kuu, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika shule zao, wametakiwa kusiimamia vema matumizi ya fedha hizo, katika utekelezaji wa miradi iliyoelekezwa kwenye shule zao, kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za Umma.
Rai hiyo imetolewa na Mkururugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, wakati kikao kazi cha maelekezo ya namna bora ya usimamizia na matumizi ya fedha hizo za serikali, katika kutekelza miradi ya maendeleo, kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa, serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 600, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya mendeleo kwenye sekta ya Elimu, hivyo amewaasa wakuu hao wa shule, wakiwa ndio wasimamizi wakuu wa fedha hizo, wanalo jukumu la kusimamia utekelezaji wa fedha hizo, ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kwa kuzingatia vigezo vilivyotolewa na serikali.
Amefafanua kuwa, lengo la serikali kutoa fedha hizo ni kuboresha miundo mbinu ya shule na kuwezesha mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia shuleni, kwa adhma ya kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi, na kuongeza kuwa ni jukumu la wakuu hao wa shule, kusimamia vema miradi hiyo ili kuendana na malengo ya serikali kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.
"Serikali imetoa maelekezo ya matumizi ya fedha hizo kwa kutumia mafundi wazawa na kutumia rasilimali zinazopatika ndani ya eneo husika yaani 'forced account', nendeni mkasimamie miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa, hakikisheni miradi inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora unaoendana na thamani ya fedha, kwa kufanya hivyo, serikali itatoa miradi mingine, ambayo itatatua changamoto za miundombinu inayozikabili shule zetu, hii ni kwa manufaa ya shule zetu na maendeleo ya wananchi wa halmashauri yetu" amesisiatiza Mkurugenzi Mtambule.
Naye Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anna Urio, amesema kuwa fedha hizo, kiasi cha shilingi milioni 600, zimepangwa kutumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule saba, ikiwa shule tatu za msingi na shule nne za sekondari, pamoja na mabweni manne kwa shule mbili za sekondari za kata.
"Serikali Imeelekeza fedha kwenye shule 7 na kila shule itajenga vyumba viwili vya madarasa pamoja na samani za madarasa hayo, kwa shilingi milioni 40 kwa kila madarasa mawili ya shule husika, na upande wa fedha za ujenzi wa mabweni, yatajengwa kwenye shule mbili za sekondari za kata na kila shule itaajenga mabweni mawili kwa shilingi milioni 160 kwa kila shule". Amesema Afisa Mipango huyo.
Aidha Afisa Mipango Anna, amezitaja shule zitakazotekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa na samani ni pamoja na shule za msingi Kambi ya Maziwa, Ilboru na Olimringaringa, huku shule za sekondari zikiwa ni Kiranyi, Kiseriani, Likamba na Iking'a, na kuongeza kuwa mabweni manne yatajengwa katika shule za sekondari Einoti na Mwandeti.
Hata hivyo, walimu hao, licha ya kuishukuru serikali kwa kutoa fedha katika shule zao lakini pia wameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo, kwa kuwapa ujuzi na maaarifa ya matumzi ya fedha hizo za serikali na namna bora ya kutekeleza miradi hiyo, na kuahidi kusimamira miradi hiyo kwa ufanisi zaidi, hasa kwa kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha hizo za serikali, huku wakiweka mbele uzalendo kufuatia malengo ya serikali ya kuboresha miundombinu ya shule zao.
Mkuu wa shule ya sekondari Ilkiding'a, mwalimu Supeet Sailevu, ameweka wazi kuwa, shule yake inakabiliwa na changamoto upungufu wa vyumba vya madarasa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga shuleni hapo, na kusisitiza kuwa, anayosababu kubwa ya kutekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa, kulinga na thamani ya fedha zilizopangwa shuleni hapo.
"Fedha hizo ni muhimu sana kwa shule ya Ilkiding'a, kwa kuwa kuna upungufu wa vyumba nane vya madarasa, huku shule hiyo ikiwa na jumla ya wanafunzi 1,428 yenye kuhitaji vyumba 28 kati ya vymba 19 vilivyopo sasa, hizo milioni 53.2 zitatumika kujenga vyumba viwili na samani zake kwa gharama ya shilingi milioni 40, na shilingi milioni 13.2 kwa ajli ya ujenzi wa choo chenye matundu 12". Amefafanua Mkuu huyo wa shule
Miradi hiyo itatekelezwa katika shule za msingi Kambi ya Maziwa, Ilboru na Olimringaringa, shule za sekondari Kiranyi, Kiseriani, Likamba, Einoti na Iking'a, shule hizo zote zitatekeleza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na samani zake, huku shule ya sekondari Ilkiding'a ikitekeleza mradi wa vyumba ipviwili vya madarsa na choo.
PICHA ZA KIKAO KAZI CHA MKURUGENZI NA WAKUU WA SHULE
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.