• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Walimu 22 wa soka shule za msingi wapikwa

Posted on: June 19th, 2018

Na. Elinipa Lupembe.

Jumla ya walimu 22 wa mchezo wa soka kwa shule za msingi,  wamepata mafunzo ya siku tano, yaliyofanyika katika shule ya msingi Ngaramtoni, halmashauri ya Arusha.

Mafunzo hayo yametolewa kwa lengo la kuwajengea walimu hao uwezo wa kufundisha wanafunzi soka taaluma, linaloendana na maendeleo ya Sayansi na teknolojia.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa shirika la Future Star Accademy, Kocha Mkufunzi, Alfredd Itaeli amesema kuwa, kupitia mafunzo hayo mwalimu wamejengewa uwezo wa  kuwafundisha watoto mbinu za kisasa za kucheza soka zinazoendana na umri wao na kwa kuzingatia zaidi wakati uliopo.  

Amesema kuwa, mwalimu amefundishwa kutoka kwenye mbinu za zamani za kufundisha soka na kujifunza mbinu za kisasa, ikiwa ni pamoja na kumfanya mwalimu kuwa na mbinu zinazoendana na wakati.

 "Tunawatoa walimu kwenye soka la kuwafanyisha watoto mazoezi magumu, ya kupanda na kushuka milima, ya kuruka kichura mazoezi yanayoharibu misuli, badala yake wachezaji kufanya mazoezi yanayojenga mwili na kuimarisha misuli na mchezaji kuwa imara.

Afisa Utamaduni, halmashauri ya Arusha, Priscus Steven amewataka walimu kwenda kutumia taaluma waliyoipata, kuwafundisha wanafunzi na si kuifunika taaluma hiyo kwa kuicha kwenye makaratasi.

Aidha amewataka walimu kuvaa uhusika wa kufundisha michezo hasa wawapo uwanjani kwani haiba ya mwalimu huwajenga watoto zaidi.

"Walimu vaeni uhusika wakati wa kufundisha soka, unapokuwa uwanjani vaa mavazi ya michezo, unakuta mwalimu anawafundisha watoto amevaa jeans, hii haikubaliki na inapunguza morari ya michezo kwa watoto" amesema Afisa huyo.

Hata hivyo walimu hao wamekiri kujifunza mbinu mpya za ufundishaji wa soka, mbinu zinazoendana na umri wa watoto, aina ya mazoezi ya kujenga pamoja na muda sahihi wa kufanya mazoezi.

Mwalimu wa soka,  shule ya Msingi Olmotony, mwalimu Aziza Laizer, amesema kuwa, mafunzo hayo yamewatoa kwenye mbinu za kizamani walizokuwa wanatumia kufundisha watoto na kuwajengea mbinu za kisasa ambazo wanaamini zitasaidia kuwajenga wanafunzi kwenye soka taaluma.

Kadhalika, mwalimu wa michezo, shule ya msingi Loovilukuny, Severine Rock, amekiri walimu wengi wa michezo kufundisha kwa uzoefu bila mafunzo yoyote huku wakitumia mbinu za kizamani, mbinu ambazo haziendani na umri wa wanafunzi na muda.

 "Walimu wengi wa michezo wanatumia uzoefu tuu, kufundisha soka lakini kupitia mafunzo hayo nimejifunza mbinu mpya na nimeweza kutambua kuwa nilikuwa nawafundisha watoto soka  bila kuzingatia muda wala umri wa watoto" amesema mwalimu Rock.      

Mafunzo hayo yamedhaminiwa na shirika la Ace Africa kwa kushirikiana na Future Star Accademy mashirika yanayosimamia mchezo wa soka kwenye shule 11 ndani ya Tarafa ya Mukulat, halmashauri ya Arusha.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA NAFASI ZA UDEREVA TAREHE 28/12/2018 December 19, 2018
  • Orodha ya majina ya walioitwa kwenye Usahili siku ya Ijumaa tarehe 20/04/2018. April 13, 2018
  • Matokeo ya usaili wa kuandika, nafasi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji Arusha DC April 20, 2018
  • Zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Taifa- NIDA kata ya Kiranyi April 20, 2018
  • Tazama zote

Habari mpya

  • Waziri Lugola akumbusha Jeshi la Polisi Arusha DC matumizi sahihi ya sheria

    February 16, 2019
  • *YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LA KUWASILISHA TAARIFA ZA KATA ROBO YA PILI, OKTOBA MPAKA DISEMBA 2018*

    February 15, 2019
  • *YALIYOJIRI ZIARA YA KATIBU MWENEZI CCM TAIFA - ARUSHA DC

    February 14, 2019
  • Wajumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango waridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo

    February 12, 2019
  • Tazama zote

Video

JPM aagiza watalamu wa Ardhi kuanzia ngazi ya halmashauri kusimamiwa na Wizara
Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.