• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

KIDATO CHA SITA WATAKIWA KUONDOA HOFU YA CORONA WAKATI HUU WA KUJIANDAA NA MITIHANI YA TAIFA

Posted on: June 1st, 2020

Na Elinipa Lupembe.

     Wanafunzi wa kidato cha sita halmashauri ya Arusha wametakiwa kuondoa hofu ya kupata maambukizi ugonjwa wa Corona, badala yake kuchukua tahadhari zinazoelekezwa mamlaka za afya, huku wakielekeza jitihada zaidi kwenye masomo, tayari, kwa kujiandaa na mitihani ya taifa inayotarajia kuanza  tarehe 29, Juni 2020.

      Rai hiyo imetolewa na Afisa Elimu Sekondari, halmashauri ya Arusha, mwalimu Menard Lupenza, wakati alipotembelea baadhi ya shule za sekondari na vyuo, katika siku ya kwanza ya masomo, na kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha sita, mara baada ya serikali kufungua shule hizo.

       Amesema kuwa, pamoja na changamoto ya ugonjwa wa Corona, maisha ya kila mtu lazima yaendelee na ndoto za wanafunzi hao lazima zitimie pia, huku akiwataka kutumia muda huu mfupi uliobaki, kujiandaa na mitihani kwa kusoma kwa bidii sambamba na wakijikinga na ugonjwa wa Corona.

        "Tunaamini mambo mengi mlikuwa tayari mmefundishwa na mlikuwa mmnajianda na mtihani huu, fanyeni marudio ya mambo yote mliyofundishwa, sikilizeni walimu wenu, fuateni maelekezo yao bila kupoteza muda, hatimaye mtafaulu mitihani yenu ya mwisho" amesema Afisa Elimu huyo.

       Aidha amewataka walimu na watumishi wa shule kujitoa kwa moyo kuwaelekeza na kuwasimamia wanafunzi kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona, kwa kuwasimamia kunawa mikono kila wakati huku wakiwafundisha kwa bidii, watieni moyo wanafunzi hawa, kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.

     Mkuu wa shule ya sekondari Ilboru George Otieno, amesema kuwa, jumla ya wanafunzi 120 kati ya 147 wameripoti shuleni hapo mpaka jana, na kukuta mazingira rafiki ya kujisomea yanayowezesha wanafunzi kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virus vya Corona.

        Ameeleza kuwa tayari vifaa vya kunawia mikono vimewekwa  maeneo yote muhimu, wanafunzi wote wamevaa barakoa, wamepunguza idadi ya wanafunzi darasani kwa kukaa  umbali wa mita moja kati ya wanafunzi mmoja na mwingine pamoja na kutenga dakika 30 za kufanya mazoezi kila siku.

      Christopher Kaduma, mwanafunzi wa kidato cha sita, ameishukuru serikali kwa kuweka mazingira salama ya kujifunzia, jambo ambalo limewaondoa hofu na kujengewa hali ya kujiamini na kuahidi kutumia muda huu mfupi kujiandaa na mitihani ya taifa huku akiwa na imani ya kufaulu kwa kiwango cha juu.

   Hata hivyo ziara Afisa Elimu huyo aliambatana na Maafisa Afya na Afisa Ustawi wa jamii, waliwaelekeza wanafunzi namna bora ya kunamikono pamoja na kutoa ushauri wa kuwa sawa kisaikolojia.

Afisa Elimu Sekondari, halmashauri ya Arusha, akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita, shule ya sekondari Bishop Danning, na wanachuo cha Ualimu Bishop Dunning, kata ya Moivo.

Wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Bishop Danning, na wanachuo cha Ualimu Bishop Dunning kata ya Moivo, wakisikiliza maelekezo ya Afisa Elimu na watalaam wa Afya siku ya kwanza ya kufungua shule.


Wanafunzi wa kidayo cha sita shule ya sekondari Ilboru, wakisikiliza maelekezo ya Afisa Elimu na watalaam wa Afya siku ya kwanza ya kufungua shule.


Afisa Afya na Elimu Shuleni, halmashauri ya Arusha, Niah Mtaki, akiwaelekeza wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Bishop Dan, namna bora ya kunawa mikono.

Wanafunzi wa kidayo cha sita shule ya sekondari Winning Spirit, wakisikiliza maelekezo ya Afisa Elimu na watalaam wa Afya siku ya kwanza ya kufungua shule.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.