• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi Arusha DC watakiwa kuwa na tabia chanya za Afya ili kufaidi maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano

Posted on: November 5th, 2019

Wananchi halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuwa na tabia chanya za afya, za kuzingatia usafi wa mazingira na usafi wao binafsi,  kwa kuwa na vyoo bora na tabia inayoendana na matumizi sahihi ya vyoo na unawaji mikono kwa sabuni katika nyakati tano  muhimu.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Tarafa ya Muklat Hudhaifa Rashid, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, wakati wa Tamasha la Uzinduzi wa kuhamasisha mbinu shirikishi ya tabia chanya za Afya, tamasha lililofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya  Daladala Ngaramtoni, mwishoni mwa juma iliyopita

Afisa Tarafa huyo amesema, lengo la Serikali ni kuwa na Taifa lenye watu wenye afya bora, afya zinazolindwa na watu wanaojali afya zao wenyewe, kwa kuwa na tabia chanya za afya, ili kuondokana na  magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa gharama ndogo, gharama ya  kubadili tabia.

Amesema kuwa asilimia 70 ya magonjwa yanayowasumbua watanzania,  yanatokana na kutokufuata tabia chanya za afya, ambazo husababisha, uchafu wa mazingira na uchafu binafsi, jambo ambalo watu wakibadili tabia magonjwa hayo yanaweza kutoweka, na kuendelea kupambana na masuala mengine ya maendeleo na si suala la usafi.

Amezitaja tabia chanya za afya ni pamoja na matumizi sahihi ya vyoo, kunawa mikono katika nyakati muhimu,usafi wa vyakula na matumizi ya maji safi na salama ya kunywa, na kufafanua kuwa, nyakati tano muhimu za  kunawa mikono ni pamoja na  baada yakutoka chooni, kabla ya kula, kabla ya kuandaa chakula,kabla ya kumnyonyesha mtoto na baada ya kumsafisha mtoto aliejisaidia (kunya)

Rashid amesisitiza kuwa, kama Serikali inatumia nguvu kubwa, kuwekeza kwenye maendeleo ya kiuchumi ni vema wananchi wakabadili tabia ili kuepuko vifo vinavyoweza kuzuilika, na baadaye kuweza kufaidi matunda ya maendeleo yanayofanywa na serikali yao ya sasa ya awamu ya tano.

"Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Dr. John Pombe Magufuli, inaweka juhudi kubwa kuboresha huduma za jamii, hivyo ni wajibu wetu sasa kuhakikisha tunafaidi matunda hayo, kwa kuwa na taifa kenye watu wenye afya bora" amesema Rashid.

Naye Naivasha Lukas, mkazi wa Ngaramtoni amesema kuwa, kwa sasa wananchi wengi wamefahamu umuhimu wa kuwa na choo bora pamoja na matumizi yake, tofauti na hapo awali, kutokana na tamaduni zao, hakukuwa na umuhimu na kuthibitisha kuwa, kampeni ya Nyumba ni Choo, imewafumbua macho na zaidi imewesha kaya nyingi kuwa na vyoo kwa sasa.

Naye Afisa Afya, halmashauri ya Arusha, Issa Msumari amesema kuwa, halmashauri inatekeleza kampeni ya kitaifa ya Usafi wa Mazingira, kampeni iliyoleta matoke chanya, mpaka sasa asilimia 73 ya kaya  ndani ya halmashauri hiyo zina vyoo.

Mpaka kufikia aslimia 73 ya kaya zenye vyoo bira, asilimia 24 kaya zenye vyoo vya asili na kufikisha asilimia 98 ya kaya zenye vyoo ndani ya halmashauri hiyo.

Hata hivyo, Afisa Afya huyo, ameweka wazi kuwa, kampeni ya kitaifa ya Usafi wa Mazingira,  imewezesha halmashauri kufikisha asilimia 98 ya kaya  kuwa na vyoo,kupitia mkakati wa kuunda kamati za ufuatiliaji katika ngazi za Vitongoji,  na kuongeza kuwa mpaka kufikia mwaka 2020, kaya zenye vyoo vya asili zitakuwa na vyoo bora na kaya zisizo na vyoo kuwa na vyoo.

Tamasha hilo liliambatana burudani mbalimbali pamoja na utoaji wa zawadi kwa washindi watano wa usafi wa mazingira kati ya kata 27 za halmashauri ya Arusha, ambapo kata ya Oloirien iliibuka kidedea, na kufuatiwa na kata ya Ilikiding'a, kata ya Olmotonyi, kata ya Lemanyata na  kata ya  Moivo likiwa na kaulimbiu inayosema 'Usichukulie Poa, nyumba ni Choo'

Awali Tamasha hilo, limefanikishwa na halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na wadau wa shirika la WaterAid-Tanzania, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wz mradi wa maji wa vijiji vitano, uliofadhiliwa na DFID.

Afisa Tarafa ya Mukulat, Hudhaifa Rashid akizungumza kwenye Tamasha la mbinu maalumu za kuhamasisha tabia chanya za afya, kwenye viwanja vya Stendi ya Daladala Ngaramtoni.







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.