Kufuatia mkakati wa Serikali kuendelea kuboresha huduma za afya, na kuhakikisha huduma hizo, zinawafikia wananchi wote hadi waishio vijijini kwa kuimarisha miundombinu ya majengo, upatikanaji wa dawa muhimu, vifaa tiba pamoja na uwepo wa wahudumu wa afya.
Wananchi wa kata ya Lemanyata halmashauri ya Arusha, wamekiri kunufaika wa huduma bora za afya zinazopatikakana kwenye kituo chao cha Afya cha Olkokola, kituo kinachotoa huduma kwa saa 24 sasa.
Aidha wamesema kuwa, kwa sasa jamii yao imepana mwanga na imeanza kubadili mtazamo juu ya Afya ya uzazi, kwa kuhimiza wajawazito na watoto wa chini ya miaka mitano, kuhudhuria kiliniki huku wanaume nao wakianza kwenda na wenzi wao kliniki, jambo ambalo hapo awali hakuwezekana kulinga na mila na desturi zao.
Naishooki Loishiye(39) mama mwenye watoti kumi, amethibitisha kuwa kabla ya kituo hicho kimeleta mabadiliko chanya kwa wananchi wa Olkokola, kwani hata yeye ifadi kubwa ya watoto wake alijifungulia nyumbanu jambo ambalo amegundua ni hatari kwa maisha yake.
Hata hivyo Wameishukuru Serikali ya awamu ya tano, iliyosababisha upatikanaji wa huduma rafiki kwa wagonjwa, uwepo wa dawa zote muhimu tofauti na hapo awali, jambo limesababisha kina mama kuacha kujifungulia nyumbani, na kuwapunguzia vifo visivyo vya lazima kwa kina mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua.
Mganga Mfawidhi kituo cha Afya Olkokola Dkt. Ezekiel Jacob, amekiri kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa kutuoni hapo mpaka kufikia wagonjwa 700 kwa mwezi na zaidi ya asilia 90 wanapata matibabu na huduma stahiki.
Shime wananchi wote tuunge mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kulipa kodi na kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yetu kwa ajili yetu na Taifa letu kwa ujumla.
Stoo ya Dawa Kituo cha Afya Olkokola
Wakibaba wakiwapeleka watoto wao Kliniki kwenye Kituo cha Afya Olkokoka (majina tunayo)
Mganga Mfawidhi, Kituo cha Afya Olkokola Dkt. Ezekel Jacob akimuhudumia mgonjwa aliyelazwa kwenye Kituo cha Afya Olkokola.
Vifaa tiba kwenye chumba wazazi (Labour ward) kituo cha Afya Olkokola
Baadhi ya Wagonjwa wakiwa Kituo cha Afya cha Olkokola kwa ajili ya kupata huduma
Mhudumu wa Afya akitoa Elimu ya Afya ya Uzazi kwa wateja waliofika kwenye Kituoncha Afya Olkokola
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.