Timu ya Ulinzi na Usalama wa mtoto Halmashauri ya Arusha imepiga marufuku kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 kwenda kwenye kumbi za starehe nyakati za usiku.
Marufuku hiyo imetolewa wakati wa kikao chakupitia utekelezaji wa shughuli za ulinzi na usalama wa mtoto Halmashauri ya arusha kwa kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2017.
Hata hivyo timu hiyo inatekeleza sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2009 inayozuia kumtumia mtoto kwa shughuli yoyote inayofanyika kwenye kumbi za starehe hasa nyakati za usiku.
Aidha sheria hiyo imefafanua kuwa mtoto yoyote haruhusiwi kuingia kwenye kumbi za starehe kama klabu zinazopiga mziki nyakati za usiku.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.