Waziri wa Maji,Mhe. Prof. Makame Mbarawa, amewahakikishia wananchi wa maeneo ya Lengijave kupata maji safi na salama, kama ilivyo adhma ya Serikali ya awamu ya tano, kufikisha huduma za maji kwa wananchi wa vijijini.
Waziri Mbarawa, amesema hayo, wakati alipotembelea na kukagua mradi wa maji wa vijiji vitano, halmashauri ya Arusha kwa uliofadhili wa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa Uingereza 'DFID', na kutekelezwa na shirika la WaterAid.
Kauli hiyo ya Waziri wa Maji, imekuja baada ya Diwani wa Kata ya Lengijave, Mhe. Kalanga Laizer, kuomba mtandao wa maji, kuongezwa ili kuwafikia wananchi wote, kutokana na utekelezaji wa Mradi huo, kutokuwafikia baadhi ya maeneo, nakuongeza kuwa wananchi hawa wanachangamoto ya maji yenye madini ya Floraidi.
Waziri Mbalawa, amesema anatambua changamoto nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maji, ikiwa ni Wasanifu wa miradi na wakandarasi, lakini Wizara ya Maji, imejipanga sasa kutekeleza miradi ya maji kwa kutumia 'forced account' na watalamu wa ndani, jambo ambalo litawezesha miradi mikubwa kutekelezwa kwa gharama ndogo, na mtandao wa maji kuwafikia wananchi wengi, katika maeneo yao.
"Ninajua wananchi wa maeneo haya wanapata maji yenye madini ya Floraidi, lakini niwahakikishe, wanachi wote wa maeneo haya watapata maji safi na salama, kupitia miradi ya wizara itakayotumia forced account, nawasihi pia tutunze miundombinu ya maji na vyanzo vya maji, tusipovitunza tutakuwa tunapoteza fedha hizi tunazotekelezea miradi hii" amesisitiza Waziri huyo wa Maji.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amemuagiza Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, kuwashughulikia wale wote wanaohujumu na kuharibu miundombinu ya maji, katika mradi huu, na kumtaka kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.
Lomunyaki Laizer, mkazi wa Lengijave, licha ya kuishukuru serikali kwa mradi huo wa maji, amesema kuwa, uhaba wa maji Lengijave, unaathiri uchumi wa familia zao, kwani wakina mama hutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.
Awali, mradi wa maji wa Vijiji Vitano, umesanifiwa kutumia teknolojia bunifu ya malipo ya kabla, ili kuwezesha jamii kupata huduma endelevu ya maji safi na salama kwa kutumia mitambo maalumu ya kuchuja maji, na kuhudumia wananchi elfu 23 kwa sasa na kufika hadi wananchi elfu 50, ifikapo mwaka 2039.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.