Zaidi ya watu 400 katika halmashauri ya Arusha,wilayani Arumeru wamepata huduma ya mbalimbali matibu ya macho, katika zoezi la upimaji wa macho lililofanyika kwa wa siku nne mfululizo, kueleea kilele cha maazimisho ya siku ya Huduma za Macho Duniani, maazimisho yaliyifanyika kimkoa katika kituo cha afya cha nduruma wilayani humo.
Zoezi hilo la matibabu ya macho limepokelewa kwa mwitikio mkubwa na wananchi wa kata ya Nduruma na vitongoji vyake, pamoja na kata za jirani za mlangarini na Bwawani kutokana na huduma hiyo kutokupatikana katika maeneo hayo.
Akifunga kilele cha maadhimisho hayo, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, Afisa Tawala wa wilaya hiyo, Mushashu Anaclet amesema kuwa, licha ya huduma za macho zinazotolewa katika viwanja hivyo lakini lengo kuu la maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kutunza macho ili kuepuka upofu unaozuilika pamoja na kuonyesha hali halisi ya magonjwa ya macho nchini na duniani.
Ameongeza kuwa takwimu za magogonjwa ya macho kwa mkoa wa Arusha mwaka 2017, zinaonyesha kuna tatizo la mtoto wa jicho kwa asilimia 90, shinikizo la jicho asilimia 2 na tatizo la trakoma lipo kwa asilimia1.2, huku halmashauri ya Arusha vijijini ikikabiliwa na tatizo la mtoto wa jicho kwa asilimia 27, kovu kwenye kioo cha jicho asilimia 35 na trakoma asilimia 1.
Aidha Anaclet amewashauri wananchi k,uacha kutumia mitishamba kutibu macho, badala yake wafike kwenye vya kutolea huduma ya ayfya pindi wanapohisi wana matatizo ya macho, kwani imegundulika kuwa, miti shamba inaweza kusababisha makovu kwenye kioo cha jicho na hatimaye kusababisha upofu.
"Niwashauri wananchi wenzangu acheni kutumia miti shamba kutibu matatizo ya macho miti shamba inasababisha makovu ambayo mwisho wake yanasababisha upofu, nendeni hospitali mkatibiwe na wataalamu kupitia vipimo vya kisasa na upatiwa vipimo sahihi kulingana na tatizo ulilonalo msicheze na jicho kwani jicho nikiungo kisicho na mbadala" amesema mgeni rasmi huyo.
Hata hivyo amewataka wale wenye uhitaji wa miwani kwaajili ya kuona vizuri waende katika hospitali zilizosajiliwa ili wafanyiwe vipimo sahihi na kupewa miwani kulingana na vipimo vyao na sio kupata huduma mitaani.
Naye Mratibu wa macho na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, mkoa wa Arusha Dkt. Mwanahawa Kombo amesema kuwa zoezi hilo limepata mafanikio makubwa, kwani walilenga kutoa matibabu kwa wananchi 200 badala yake, kumekuwa na mwitikio mkubwa hadi sasa tayari wametibiwa wananchi takribani 400 jambo ambalo limesababisha kuvuka malengo.
Aidha amezitaja huduma za macho zinazotolewa kituoninhapo ni pamoja na kupima macho, kutoa dawa kwa wale wenye kuhitaji tiba, kupima macho kwa wagonjwa wa kisukari, kufanya upasuaji mdogo wa vikope, kutoa miwani kwa watu wazima kuanzia miaka 40 na kuendelea kwa ajili ya kuonea karibu, kutoa ushauri kwa wagonjwa, sambamba na kutoa rufaa kwenda hospitali ya rufaa KCMC kwa wagonjwa ambao wanahitaji huduma za matibabu zaidi.
Hata hivyo Dkt.Mwanahawa amethibitisha kuwa wagonjwa ishirini, waliogundulika na tatizo la mtoto wa jicho, watafanyiwa upasuaji katika hospitali ya St. Elizabeth kwa ufadhili wa shirika la Kilimanjaro Center for Community Ophthalmology (KCCO) huku wagonjwa wengine waliokutwa na ugonjwa wa vikope wakitolewa pale pale.
Ameongeza kuwa licha ya kujikita zaidi kwenye matibabu ya macho lakini pia wananchi wamepata fursa ya kupima magonjwa mengine ikiwemo kisukari,shinikizo la damu, virusi vya UKIMWI pamoja na kansa ya matiti kwa wanawake.
Kwa upande wao wananchi waliopatiwa huduma hiyo wameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli, kwa kuwajali wananchi wake hasa waishio vijijini, na kuwapelekea huduma hiyo ya matibabu ya macho huduma ambayo haijawahi kupatikana katika eneo hilo.
Joshua Lekeiya mwananchi wa kijiji cha maji moto baada ya kupimwa na kupatiwa miwani ya kusomea amekira kufurahishwa na huduma hiyo iliyoletwa karibu nao na kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kusema kuwa wananchi wengi sasa hasa wa vijijini wanapata huduma nyingi tofauti na hapo awali walikuwa wakizisikia tu zikitolewa mjini.
"Kiukweli sisi wananchi wa hali ya chini tunafurahishwa sana na kitendo cha serikali kutuletea huduma hadi vijijini, Mimi sikuamini kama ni kweli lakini nimefika hapa kituo chetu cha nduruma nimepimwa macho na nimepewa Miwani ya uoni hafifu na nimeshudia wenzangu wakipata huduma mbalimbali za afya ya macho" .amesema Lekeiya
Siku ya Afya ya macho duniani huadhimishwa kila alhamisi ya pili ya mwezi wa kumi na katika mkoa wa Arusha maazimisho yamefanyika katika kata ya Nduruma, halmashauri ya arusha wilayani Arumeru yenye kauli mbiu ya Kauli mbiu 'Afya ya macho kwa wote huduma za macho popote ulipo'.
*PICHA ZA MATUKIO KWENYE KILELE CHA SIKU YA MACHO DUNIANI*
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.