Na. Elinipa Lupembe.
Zoezi la kitaifa la kubaini kaya zenye vigezo vya kuingia kwenye mpango wa Kunusuru kaya masikini, katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi unaotekelezwa na TASAF awamu ya tatu kwa mwaka 2020-2025, limeanza rasmi katika vijiji 43 vya halmasahuri ya Arusha, vijiji ambavyo havikuwa kwenye mpango katika awamu ya kwanza ya mradi huo.
Jumla ya wawezeshaji 43 (PAA FACILITATOR) wametawanyika katika vijiji hivyo 43, wakielekeza viongozi ngazi ya vijiji na vitongoji pamoja na wananchi vigezo vya kuziibua kaya hizo, kwa kuzingatia vigezo vya kitaifa na vigezo vya na vigezo vya eneo husika, zoezi linalofanyika kupitia mikutano ya serikali za vijiji na mikutano maalumu ya vijiji, huku vigezo vya upimaji vikiwekwa wazi kwa kila mwananchi
Katika maeneo mengi ya vijiji husika, wananchi wamejitokeza kwa wingi, kushiriki zoezi hili muhimu kwao, lenye lengo la kuziibua kaya hizo na kuziwesha kaya zisizo na uwezo wa kujikimu kimaisha, kuingizwa kwenye mpango wa serikali wa kupambana na umasikini kwa kuziwezesha kaya hizokujiinua kimaisha pamoja na kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini uliokithiri kwenye jamii.
Hata hivyo baada ya kaya hizo kupitishwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa kijiji, wawezeshaji watalazimika kupita kwenye makazi ya kaya zilizoibuliwa (kaya kwa kaya), ili kuorodhesha majina ya wanakaya hao pamoja na kudodosa hali halisi za kijamii na kiuchumi za kaya hizo, lengo likiwa ni kujiridhisha na uwepo wa kaya hizo katika eneo husika.
Zoezi hilo la wazi na linategemea kufanyika kwa takribani siku kumi kwenye vijiji hivyo vya halmashauri ya Arusha, hivyo wananchi ambao majina yao yatapitishwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji na Vitongoji, watalazimika kutoa ushirikiano mkubwa kwa wawezeshaji hao, ili kupata kaya zenye vigezo halisi vilivyoainishwa na si vinginevyo, ili kuepuka malalamiko sambamba na kutimiza adhma ya serikali ya kupambana na umasikini katika jamii ya watanzania.
Aidha kaya zitakazoibuliwa zinatakiwa, kuwepo nyumbani kwa zile siku zilizokubalika na viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na wawezeshaji wa TASAF, ili kaya hizo ziweze kutoa taarifa sahihi za kaya zao, ikiwemo idadi ya wanakaya, majina sahihi ya wanakaya, majina sahihi ya shule wanazosoma watoto wao, majina shahihi ya vituo vya afya wanavyotumia kupelekwa watoto wanaohudhuria kliniki, watoto wenye umri wa mwaka sifuri mpaka miaka mitano.
ARUSHA DC KAZI INAENDELEA✍✍
Mwenyekiti wa kijiji cha Ilkerini mheshimiwa Sanaek Soye, akifungua mkutano maalumu wa kijiji, tayari kwa uibuaji wa kaya za kuingiwa kwenye mradi wa Mapngo wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF awamu ya tatu 2020 -2025.
Wananchi wa kitongoji cha Parselian kijiji cha Ilkerin, wakiwa tayari kuanza kutaja majina ya kaya zenye sifa za kuingizwa kwenye awamu ya pili ya mradi wa kaya maskini TASAF awamu ya tatu, zoezi lililofanyika wakati wa mkutano maalum wa kijiji cha Ilekerin kata ya Kisongo.
Mjumbee wa serikali ya kijiji cha Ilkerini kata ya Kisongo (jina halikuweza kuapatikana) akiwaelezea wananchi wa Ilkerin umuhimu wa kuibua kaya zenye sifa, wakati wa mkutano maalumu wa kijiji wa kuibua kaya zenye uhitaji kuingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini.
Wananchi katika mkutano wa kijiji cha Engutukoiti kata ya Losinoni.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Engutukoiti wakiwa kwenye mkutano wa kijiji.
Wajumbe wa serikali ya kijiji cha Engutukoit kata ya Losinoni wakilamkiapo cha utii wa kusimamia kazi ya uibuaji kaya zenye uhitaji katika kijiji chao.
Mwezeshaji akiendelea kutoa maelekzo kwa wananchi juu ya uibuji kaya za kuingiankwenye mradi wa kunusuru kaya masikini na TASAF awamu ya tatu, kwenye Mkutano wa wananchi wa kijiji cha Likamba kata ya Musa
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.