• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ARUSHA DC

Posted on: May 25th, 2022

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha amepokea kibali cha kutekeleza Ikama na Bajeti kwa Ajira Mpya kwa mwaka wa fedha 2021/2022 chenye Kumb.Na. 97/228/01/9 cha tarehe 13 Mei, 2022 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha anawatangazia wananchi wote ambao ni Raia wa Tanzania wenye sifa kuomba nafasi zilizoorodheshwa hapa chini:-

  • MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 10   - TGS B
  • SIFA ZA MWOMBAJI:
  • Awe amefaulu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI)
  • Awe amefuzu mafunzo ya Astashahada (Cheti) NTA level 5’ kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:-
  • Utawala
  • Sheria
  • Elimu ya Jamii
  • Usimamizi wa Fedha
  • Maendeleo ya Jamii
  • Sayansi ya Jamii

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI

  • Katibu wa Kamati ya Kijiji
  • Mtendaji Mkuu wa Kijiji
  • Mratibu wa utekelezaji wa sera na sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Kijiji.
  • Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Kijiji.
  • Msimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogo pamoja na sheria nyingine zinazotumika katika Kijiji.
  • Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu masuala ya ulinzi na usalama.
  • Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini katika Kijiji.
  • Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote katika Kijiji.
  • Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Kijiji atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
  • DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 4  - TGS B
  • SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe amefaulu kidato cha nne (iv) au cha sita (vi).
  • Leseni ya daraja E au G ya Uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
  • Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.

MAJUKUMU YA KAZI YA UDEREVA:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari na;
  • Kufanya kazi nyingine kadri utakavyoelezwa na Msimamizi wa kazi.
  • KATIBU MAHUSUSI DARAJA III (NAFASI 3):       - TGS B
  • SIFA ZA MWOMBAJI:
  • Awe amefaulu kidato cha nne (iv)
  • Awe amehudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu hatua ya tatu  kutoka kwenye Chuo cha Utumishi wa Umma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
  • Awe amefaulu somo la hati mkato ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na cheti cha programu ya windows, Microsoft office, Internat-E-mail na Publisher.

KAZI NA MAJUKUMU YA KATIBU MAHUSUSI

  • Kuchapa taarifa na nyaraka za kawaiida.
  • Kupokea wageni na kuwasaidia shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikia.
  • Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada na nyaraka mbalimbali.
  • Kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake.
  • Kupokea majalada, kuyagawa kwa Maafisa kufanya kazi zozote atakazopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

MASHARTI YA UJUMLA:

  • Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45
  • Mwombaji aambatanishe nakala ya kadi ya NIDA
  • Mwombaji aambatanishe cheti cha kuzaliwa
  • Mwombaji aambatanishe maelezo yake binafsi (CV) pamoja na namba za simu zinazopatikana muda wote
  • Mwombaji awe na wadhamini watatu na namba za simu ambazo zinazopatikana muda wote
  • Mwombaji wakati wa kuwasilisha maombi aweke picha ndogo (Passport size) moja iliyoandikwa jina kwa nyuma na ibandikwe kwenye barua ya maombi.
  • Barua ziandikwe kwa mkono  na ziambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu pamoja na taaluma.
  • Testimonial, Provisional result, statement of result HAVIKUBALIKI
  • Waombaji wote ambao wamesoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimefanyiwa ulinganishi na TCU na NACTE na kuambatanisha taarifa kutoka Mamlaka husika.
  • Madereva waambatanishe maombi la Leseni ya udereva.
  • Waombaji wote watatakiwa kuangalia mara kwa mara kwenye tovuti wa Halmashauri kwa sababu watakaoitwa kwenye usaili wa awali majina yao yatawekwa kwenye tovuti ya Halmashauri  ambayo ni www.arushadc.go.tz”
  • Mwisho wa kutuma maombi  ni tarehe 07.06.2022.
  • Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili “HAYATAFIKIRIWA”.
  • MAOMBI YOTE YATUMWE KWA NJIA YA POSTA KATIKA ANUANI IFUATAYO:
  • MKURUGENZI MTENDAJI,
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA,
  • S.L.P 2330,
  • ARUSHA.

Seleman H. Msumi

MKURUGENZI MTENDAJI (W)

 

Nakala:       1.       Katibu,

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,

S.L.P. 2320,

DODOMA

2.       Website :www.arushadc.go.tz

3.       Mbao Zote za Matangazo.


Matangazo

  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022 tarehe 09.05.2022 May 08, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA ARUSHA DC,BW.SELEMAN MSUMI AKIWA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO KATIKA MASDHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA ARUSHA

    May 02, 2025
  • HERI YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • HERI YA SIKU YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • MHE. MAJALIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.