Friday 9th, May 2025
@UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA DC
TAARIFA KWA UMMA/VYOMBO VYA HABARI.
Halmashauri ya Arusha inategemea kufanya Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani wa robo ya pili mwaka wa fedha 2022/2023, kwa kipindi cha kuanzia Oktoba mpaka Desemba 2022. Mkutano huo utafanyika tarehe 01.03.2023 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo, kuanzia saa 03:00 asubuhi.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali za Mitaa, ukiwa na Agenda 10 huku Agenda kuu zikiwa ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo, taarifa ya Mapato na Matumizi ya mwezi Desemba 2022, Taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya robo ya pili za Halmashauri, Wakala wa Barbara Mijini na Vijijini (TARURA), Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Wakala wa Umeme Vijijini (REA), pamoja na Kupitisha Mihtasari ya Vikao vya robo vya Kamati za nne za Kudumu.
Aidha Mkutano Baraza la Madiwani ni Mkutano wa wazi, hivyo wananchi wote wa Halmashauri ya Arusha wanatakiwa kuhudhuria, ili kufuatilia kwa uwazi shughuli za utekelezaji wa Maendeleo zilizotekelezwa katika Halmashauri yao kwa kipindi cha miezi mitatu na robo ya pili, mwaka wa fedha 2022/2023.
Imetolewa na:-
Elinipa J. Lupembe.
KAIMU MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.