Friday 29th, March 2024
@MKUTANO WA BARAZA LA TAARIFA ZA KATA
MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO ZA KATA KWA ROBO YA KWANZA 2O22/2023 KUFANYIKA TAREHE 03.11.2022
MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO ZA KATA KWA ROBO YA KWANZA 2O22/2023
Halmashauri ya Arusha inatarajia kufanya Mkutano wa Baraza la Madiwani la kuwasilsiha taarifa za Utekelezaji Wa Shughuili za Maendeleo za Kata kwa robo ya kwanza mwaka wa fedha 2022/2023, kuanzia Julai mpaka Septemba 2022.
Aidha Mkutano utakaofanyika tarehe 03.11.2022 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo, kuanzia saa 03:00 asubuhi na utakuwa na ajenda 6 ambapo agenda kuu ni kuwasilsiha taarifa za kata zote 27 za halmashauri ya wilaya ya Arusha.
Mkutano huu ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria za Serikali za Mitaa, ambao unatoa nafasi kwa Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza.
Taarifa hizo zinajumuisha shughuli za maendeleo zilizofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kisekta pamoja na mipango endelevu ya kata husika.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji halamsaghuri ya Arusha Selema \Msumi anawakaribisha wananchi wote wa Halmashauri ya Arusha Kuhudhuria Mkutano huo unaojadili Maendeleo ya Halmashauri yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.