• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO..

Posted on: March 14th, 2023


Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema utunzaji siri za Serikali ni jambo muhimu huku akiwataka Wakuu wa Wilaya kuacha kutumiana nyaraka za Serikali kwa kutumia mitandao ya kijamii au barua pepe binafsi.


Akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara leo Machi 13, 2023 kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi hao kuwachukulia hatua watumishi wazembe, wabadhirifu na wanaokwamisha miradi ya Serikali katika maeneo yao.


“Utunzaji siri za Serikali ni muhimu sana hususani katika kipindi hiki cha utandawazi na matumizi ya mitandao ya kijamii yawapasa mzingatie kuwa siri ndio uhai wa Serikali. Hivyo, ni lazima kudhibiti uvujaji wa siri za Serikali. Epukeni kabisa kutumia mitandao ya kijamii kama whatsapp, ama email binafsi kutuma nyaraka za Serikali’ amesitiza Dkt. Mpango.


Amewataka watoa mada kuhakikisha wanasisitiza kuhusu matumizi ya walinzi binafsi (bodyguards) na Waandishi wa Habari binafsi katika Ofisi za Umma kwa kuwa zipo taratibu za umma za kupatiwa wasaidizi hao.



Dkt. Mpango amewataka viongozi hao kuhakikisha wanasimamia   maadili, nidhamu na uwajibikaji wa watumishi kwa wananchi na kuepuka lugha za matusi na kujifanya miungu watu.


“Msiende kuwa Miungu watu, nendeni mkatende haki kwa wananchi na watumishi walio chini yenu. Wahudumieni wananchi kwa staha, sikilizeni kero zao na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati. Ninyi kama Viongozi mnapaswa kuongoza kwa mfano na kuweni makini wakati wote mnapozungumza na Umma, hakikisheni mnatumia lugha fasaha na nzuri.”amesema .


“Epukeni kutoa lugha ya matusi. Aidha, mienendo yenu na muonekano wenu mbele ya jamii uwe ni wa mfano, mienendo isiyofaa kama ulevi, ufuska, unyanyasaji wa kijinsia, matumizi mabaya ya madaraka yenu, ufisadi, rushwa n.k. haiendani kabisa na dhamana mliyopewa" Dkt. Mpango.


#KaziIendelee✍✍





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.