Na ElinipaLupembe
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, ametoa maagizo kwa Mamlaka husika kupitia Mawaziri wenye dhamna kutatua kero zinazowakabili wananchi wa halmashauri ya Arusha, zilizowasilishwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Noah Lembis Saput.
Hata hivyo Mhe. Dkt. Mpango ametoa pole kwa wahanga wote wa changamoto hizo na kumuagiza Mkurugenzi wa TARURA nchini kusimamia matengenzo ya barabara za ndani za zilizoharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha katika msimu huu wa mvua zikikata mawasiliano kwa baadhi ya maeneo na kusababisha adha kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
Aidha amemuagiza Meneja wa TARURA mkoa wa Arusha kuangalia salio la bajeti na kudhibiti korongo lililo pembeni ya kanisa Katoliki Ngaramtoni, korongo linalotishia usalama wa jengo hilo na waumini wa kanisa hilo.
Dkt Mpango ameiagiza Mamlaka ya Chakula NFRA kuangalia upya namna ya kuenendelea kutoa chakula cha ruzuku kwa watu wenye uhaba wa chakula, changamoto iliyosababishwa na ukame uliyakabili eneo kubwa katika jimbo hilo.
Kadhalika, amemtaka pia Waziri wa Maji kwa kushirikina na Mkurugenzi wa RUWASA kuongeza nguvu ya kusimamia miradi ya maji katika jimbo hilo, miradi ambayo imetaarifiwa na Mhe. Mbunge huyo kutekelezwa kwa muda mrefu bila kukamilika.
Na mwisho kabisa, amemuagiza Waziri mwenye dhamana TAMISEMI kufanyia kazi ombi la kuigawa wilaya ya Arumemeru kutokana na ukubwa wa eneo hilo na wananchi kupata adha ya kufika ofisi ya mkuu wa wilaya na kupata huduma, ombi ambalo lilitolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Comredi Steven Zelothe Steven.
"Kuna gharama kubwa katika kugawa na kuongeza maeneo ya kiutawala, lakini Mkoa na TAMISEMI fanyieni kazi upya na kuangalia uwezekano wa kugawa wilaya hiyo kwa dharura kwa kuzingatia vigezo vinavyohitajika kuwa wilaya" Amefafanua Mhe. Dkt. Mpango
Awali akizungumza wakati wa kutoa salamu za wananchi wa Jimbo la Arumeru Mh. Noah licha ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi imara wa Jemadari mama Dkt. Samia Suluhu Hassani, amezitaja changamoto kubwa zinawazokabaili wananchi wa jimbo hilo ikiwa ni pamoja na uharibifu mkubwa wa barabara za ndani, uliotokana na mvua kubwa zilizonuesha katika msimu huu wa mvua, utekelezaji wa miradi ya maji kuchukua muda mrefu kukamilika na kusababisha wananchi kokosa maji kama yalivyo malengo ya serikali ya kufikisha asilimia 90 mijijini na 80 vijijini huku jimbo hilo likiwa na 65 tu.
Aidha Mhe. Noah amemuomba Makamu wa Rais, kutokana na hali ya ukame unayolikabili jimbo hilo, ameomba kuangalia upya namna ya kuendelea kuwapa chakula wananchi wa baadhi ya kata zilizokumbwa na ukame na kusababisha upungufu mkbwa wa chakula kwa baadhi ya wananchi.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
KaziInaendelea
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.