Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Arusha,Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi wote, kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani (Full Council), utakaofanyika siku ya Ijumaa, tarehe 10.08.2018, kwenye Ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Mkutano huu ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria za Serikali za Mitaa, utakaojadili shughuli za utekelezaji wa maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne na ya mwisho kwa mwaka wa fedha 2017/2018, cha kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni, 2018.
Mkutano utakuwa na agenda 17, agenga kuu ikiwa ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo, Kujadili taarifa za Mapato na Matumizi, taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kupokea na kupitisha mihitasari ya Kamati nne za kudumu za halmashauri pamoja na utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo ya Mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni.
Agenda nyinguni ni Taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa mwaka wa fedha uliomalizika wa 2017/18, Mrejesho wa Mpango wa Mapato na Matumizi kwa bajeti ya mwaka mpya wa fedha 2018/2019 pamoja na kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2018/19.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji anawataka wananchi zote kuhudhuria mkutano huo unaojadili Maendeleo ya Halmashauri yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.