Shule za Sekondari za Halmashauri ya Wilaya ya Arusha zimefanya vizuri kwenye Matokeo ya mitihani ya Taifa ya kidato cha nne kwa Mwaka 2023 yaliotangazwa na Baraza la mitihani la Taifa NACTE.
Akieleza matokeo haya Afisa Elimu Sekondari Menard Lupenza amesema ufaulu huu ni wakishindo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na inadhihirisha ufaulu wa asilimia 97.4 ikiwa ni ongezeko kubwa kwa matokeo yaliopita.
Amesema jumla ya wanafunzi wapatao 5537 wa Shule za Serikali na Shule Binafsi waliofanya mitihani hii wamweza kupata ufaulu mzuri kwenye masomo mbali mbali .
Wanafunzi waliofaulu kwa Daraja la kwanza hadi Daraja la Tatu I-III ni Jumla ya 2903 Wakiwa ni wa Shule za Serikli na Binafsi ikiwa ni sawa na asilimia 59.3 ,na Wanafunzi waliofaulu kwa Daraja la kwanza hadi Daraja la Nne I-IV ni jumla ya wanafunzi 5530 sawa na asilimia 97.3 na waliopata Daraja la Zero ni wanafunzi 173 sawa na asilia 2.7
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Arusha Menard Lupenza akielezea ufaulu wa Wanafunzi wa Kdato cha Nne 2023.
Wanafunzi wa shule za serikali waliofanya mitihani yao na ufaulu ni jumla ya wanafunzi 4738 na ufaulu wao ,Wanafunzi waliopata ufaulu wa Daraja la kwanza mpaka Daraja la nne I-IV ni wafaunzi 4566 sawa na asilimia 96.
Wananfunzi waliopata ufaulu wa Daraja la kwanza hadi Daraja la Tatu I-III ni wanafunzi wapatao 2204 sawa na asilimia 44 ya wanafunzi wote na, wanafunzi waliopata Daraja la Zero ni 172 sawa na asilimia 4.
Kwa upande wa Shule za Binafsi wanafunzi waliohitimu elimu ya kidato cha Nne ni wanafunzi 799 na ufaulu wao kwa Daraja la kwanza hadi Daraja la nne ni wanafunzi 764 sawa na asilimia 99.5 na waliofaulu ufaulu wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 669 sawa na asilimia 85 na wanafunzi waliopata Daraja la Zero ni 1 sawa asilimia 0.5.
Aidha ameelezea kuwa ufaulu huu umeongezeka kutoka asilimia 93.4 ya mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 97.3 kwa mwaka wa 2023 ,Haya ni mafanikio makubwa kwa Wilaya , Waalimu ,Wazazi na Wanafunzi kwa Ujumla.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.