Na Elinipa Lupembe
Uongozi wa halmashauri ya Arusha, umekabidhi vyeti vya pongezi na shukurani kwa wadau wa maendeleo wa halmashauri hiyo, walioshiriki kuchangia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vyeti vya pongezi, Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, mheshimiwa Ojung'u Salekwa, amewashukuru wadau hao kwa ushirikiano na kujitoa kwa moyo kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisekta wakati halmashauti ikiwa kwenye maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2022.
"Serikali inatambua na kuthamini sana michango ya wadau wa maendeleo kwa kuwa wanafanya kwa niaba ya serikali, shukrani tuliyoitoa haina thamani ya huduma mliyoitoa, ila tunaamini katika utoaji wenu wenye baraka, maandiko yanasema heri mkono unaotoa kuliko kupokea" Amesisitiza Mheshimiwa Ojung'u
Hata hivyo mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, licha ya kuwashukuru wadau hao kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo ya wananchi wa halamshauri ya Arusha na kwa taifa na kuwataka wasichoke kuendelea kuisaidia halmashauri hiyo kwa kuwa bado kuna mahitaji mengi ya kijamii ambayo serikali peke yake haiwezi kuitekelza.
Aidha Mkurugenzi Msumi, amewataja wadau hao ni pamoja na Mchungaji Philemon Olais Mollel, Michael Lembris Mollel, Eliaman Joseph Mollel, Olais Nanaya Mollel, Elibariki Kiberenge Levoyo, Diwani wa kata ya Sokon II Mhe. Elias Long'idare Mollel, Remmy William Mollel, Julius Logiru Meshuko, pamoja na shirika la Walking in Love na shirika la CWCD.
Hata hivyo wadau hao wameushukuru uongozi wa halamsahuri kwa kutambua na kuthamini michango yao na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya sita kuchangia maendeleo ya nchi.
Mchungaji Philemon Molel ameweka wazi kuwa, kwa halmashauri kutambua na kuthamini mchango walioutoa inajenga matumani na moyo wa kuendelea kutoa huku wadau wengine wakiendelea kuhamasika kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuchangia miradi ya maendeleo.
Awali uongozi wa halmashauri ya Arusha, kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa halmashauri, Baraza la waheshimiwa Madiwani na watalamu, wanawakaribisha wadau wa maendeleo kujitikeza kwa wingi kuendelea kuchangia miradi mbalimbali ya halmashauri ya Arusha.
ARUSHA DC TUPO TAYARI KUHESABIWA ✍
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUKABIDHI VYETI VYA PONGEZI
Diwani wa kata ya Sokon II, Mhe. Obedi Mollel (kushoto) kipokea cheti cha shukurani kwa kuchangia mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2022, kutoka kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mhe,. Ojung'u Salekwa wakati wa mkutano wa Baraza la madiwani kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Mchungaji Philemon Olais Mollel (kushoto) kipokea cheti cha shukurani kwa kuchangia mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2022, kutoka kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mhe,. Ojung'u Salekwa wakati wa mkutano wa Baraza la madiwani kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi wa shirika la Walking in Love (kushoto) kipokea cheti cha shukurani kwa kuchangia mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2022, kutoka kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mhe,. Ojung'u Salekwa wakati wa mkutano wa Baraza la madiwani kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Mwakilishi wa shirika la CWCD (kushoto) kipokea cheti cha shukurani kwa kuchangia mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2022, kutoka kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mhe,. Ojung'u Salekwa wakati wa mkutano wa Baraza la madiwani kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Mchungaji Philemon Olais Mollel (kushoto) kipokea cheti cha shukurani kwa kuchangia mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2022, kutoka kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mhe,. Ojung'u Salekwa wakati wa mkutano wa Baraza la madiwani kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.