• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ARUSHA DC YAZINDUA MIONGOZO YA USIMAMIZI WA ELIMU NCHINI

Posted on: September 27th, 2022

Na Elinipa Lupembe.

Mkuu wa wilaya wa Arumeru, Mhandis Richard  Ruyango amezimdua miongozo yausimamizi wa elimu nchini, iliyotolewa na serikali kupitia wizara ya elimu, tayari kwa utekelezaji katika halmashauri ya Arusha, hafla ilyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Mhandisi Ruyango, amewataka walimu kufanyakazi kwa weledi kwa kuzingatia miongozo wa elimu, iliyotolewa na serikali yenye lengo la kuimarisha utoaji wa elimu nchini na uimarishaji hali ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini.

Mkuu huyo wa wilaya ameelezea kuwa, wanufaika wakubwa wa mwongozo huo ni wanafunzi hivyo ni vyema viongozi wa ngazi zote kusimamia utekelezaji wake, na kuwasisitiza walimu kuitendea haki miongozo hiyo, kwa kuwa wao ndio watekelezaji wakuu ili kumfikia mlaji ambaye ni mwanafunzi.

"Serikali inategemea matokeo chanya ya miongozo hii, na walimu ndio watekelezaji wakuu kwa kuifanyia kazi moja kwa moja kwa wanafunzi ambao ndio walengwa, hivyo tunawategemea ninyi walimu, mnapaswa kufanya kazi kwa weledi ili kufikia malengo ya serikali". Amesisitiza Mhandisi Ruyango.

Mwongozo unaekekeza kuandikisha wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza kuanzia mwezi Oktoba na huu ndio msimu, anzeni kuandikisha watoto sasa, kusiwe na mtoto mwenye umri wa kuandikishwa shule anaachwa, mpaka kufikia mwezi Januari 2023, wote wawe wameandikishwa.

Nao wanafunzi, walioshuhudia uzinduzi huo, wameipongeza serikali kwa kuandaa miongozo hiyo, na kuthibitisha kuwa miongozo yote inamanufaa makubwa kwao, huku wakiamini serikali ina mipango thabiti kwa wanafunzi na kuinua kiwango cha taaluma nchini.

"Ninaipongeza serikali kwa miongozo hii ambayo dira yake inaelekeza wanufaika wakuu ni sisi wanafunzi, tunamshukuru mkuu wetu wa wilaya, tunamshukuru Rais wetu, mama Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha mpango wa elimu nchini, unaotunufaisha sisi wanafunzi" Amebainisha Joshua Lenatus, mwanafunzi wa darasa la 5, shule ya msingi Sekei.


Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameahidi kusimamia utekelezaji wa mwongozo huo kwa shule zote, kwa kushirikana na timu nzima ya elimu, na kuhakikisha mwongozo huo unazaa matunda yaliyokusudiwa na kufikia lengo la serikali.

Awali mwongozo wa elimu nchini umejikita katika namna ya uteuzi wa viongozi wa elimu, mkakati wa kuimarisha ujifunzaji na ufundisha unaotumia zana halisi na wanafunzi kumudu stadi za kusoma kuandika na kuhesabu, utatuzi wa changamoto katika uboreshaji elimu ya msingi na sekondari pamoja na mwongozo wa  utoaji huduma za chakula na lishe shuleni.
 

ARUSHA DC

Tupo kazini ✍✍✍


PICHA ZA MATUKIO

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, akikata utepe kitabu cha miongozo ya Elimu, kama ishara ya kuzindua miongozo hiyo katika halmashauri ya Arusha, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, akiwakabidhi  kitabu cha miongozo ya Elimu, Afisa Elimu na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiutu, mara baada ya uzinduzi wa miongo hiyo katika halmashauri ya Arusha, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, akiwakabidhi  kitabu cha miongozo ya Elimu, Afisa Elimu na Afisa Mtendaji wa Kata ya Oloirin, mara baada ya uzinduzi wa miongo hiyo katika halmashauri ya Arusha, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.


Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa miongozo ya Elimu katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha

Baadhi ya Maafisa Elimu Kata waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa miongozo ya Elimu katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha

Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango na wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa miongozo ya Elimu katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.