Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, amemuagiza mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha kusimamia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule 6 za msingi, miradi inayotekelezwa na serikali kupitia mradi wa BOOST.
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kukagua maendeleo ya utekelzaji wa miradi hiyo, huku akiwasisitiza watalamu na kamati ya usimamizi kuweka kambi kwenye miradi hiyo na kukamilika kabla ya tarehe 20.07.2023.
"Licha ya changamoto za utekelezaji wa mradi hakikisheni mnawasimamia mafunzi wote ikiwezekana wafanyekazi usiku na mchana na kufika ukamilishaji wa ujenzi kulingana na muda wa mkataba". Amesisitiza mkuu huyo wa wilaya.
Hata hivyo mkurugenzi Mtendaji Seleman Msumi amekiri kuonheza kasi ya usimamizi wa ujenzi na kufika malengo yaliyowekwa na serikali.
Ikumbukwe kuwa serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 682.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule 6 za msingi yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora kwa elimu ya awali na msingi Tanzania Bara (BOOST).
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
#kaziiendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.