Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda akikagua hali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo shule ya msingi Olokii kata ya Bwawani.
Mkuu huyo wa wilaya akiwa amembatana na Kamati ya Usalama wilaya, wamekagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu ya vyoo vilivyojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 81.3 fedha kutoka serikali kuu kupitia mradi wa kutoka Serikali Kuu kupitia kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Serikali ilianza kujenaga shule ya msingi Olokii mapema mwaka 2021 ikiwa kama shule shikizi Olmapinuu mara baada ya kufungwa iliyokuwa shule ya msingi Olokii kijiji cha Bwawani kutokana na shule hiyo kutitia kwenye tope kutokana na mafuriko.
Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C)Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.