• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED MTAMBULE ATETA NA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU ARUSHA DC

Posted on: July 10th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, amewataka watumishi wa halmashauri  hiyo, kutekeleza wajibu wao kwa kutambua majukumu yao ya kiutumishi kwa kufanyakazi kwa kujiamini huku wakisimamia maadili ya utumishi wa Umma.

Mkurugenzi Mtambule, amesema hayo alipokutana kwa mara ya kwanza na watumishi wa makao Makuu ya halmashauri hiyo, kwenye kikao  chake cha kujitambulisha, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, mara baada ya kuanza kazi  rasmi katika halmashauri hiyo, baada ya uteuzi wake uliofanywa na mheshimiwa Rais mwishoni mwa  wiki iliyopita.

Mkurugenzi huyo amewataka watumishi hao, kufanyakazi kwa bidii, huku nguzo kubwa ikiwa ni ukweli na uaminifu katika utendaji wa kazi, kwa kutanguliza utu na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku lengo likiwa ni kuwahudumia wananchi kwa maendeleo ya halmashauri ya Arusha.

Aidha amewataka watumishi hao, kuwa wabunifu katika kazi, ili kazi zao ziwatofautishe na watumishi wa halmashauri nyingine, kwa kuwa majukumu ya utumishi wa Umma yamefanana kwa halmashauri zote, tofauti inakuja katika ubunifu na kuongeza thamani katika utendaji kazi.

"Acheni kufanya kazi kwa mazoe, kuweni watumishi wa tofauti wa kubuni mambo zaidi kwenye kazi zenu, kazi za utumishi wa Umma zinalingana kote, ila ukifanya kitu tofauti kitafikisha halmashauri yetu katika hatua nyingine tofauti" amesisitiza Mkurugenzi Mtambule.

Aidha amewataka watumishi hao kuishi kama familia moja, kwa kupendana, kuelekezana, kubebeana zaidi  kufanyakazi kama timu moja kwa kuzingatia miongozo, kanuni na sheria za utumishi wa Umma.

Ameendelea kufafanua kuwa, jukumu kubwa la Watumishi  ni kutatua kero za wananchi, hivyo jipeni muda wa kuwasikiliza wananchi, kutumieni lugha nzuri yenye staa, hudumieni wananchi kwa upendo bila kuwabagua, tatueni kero zao kwa kuwambia  wananchi ukweli ili kujenga taswira nzuri ya halamashauri yetu.

"Serikali imewaamini na kuwapa jukumu la kuitumikia, tunzeni siri za ofisi na za watumishi wenzenu, hakikisha unafanya kazi kwa nidhamu, kwa kufuata maadili ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini na kutumia muda wa kazi kufanyakazi na si vinginevyo" amesema mkurugenzi huyo.

Nao watumishi wa halmashauri hiyo, wameahidi kumpa ushirikiano, mkurugenzi huyo kwa kutekeleza majukumu yao bila kusukumwa, kwa kuzingatia maafili ya utumishi wa Umma, lengo likiwa kutoa huduma bora kwa  wananchi wa halmashauri ya Arusha.

Akimkaribisha Mkurugenzi huyo kwa niaba ya watumishi wa halmashauri ya Arusha, Kaimu Afisa Utumishi, Abihud Mwakijambile, amesema kuwa, watumishi hao wako tayari kushirikiana na mkurugenzi huyo mgeni, kufanyakazi kwa bidii kama timu kwa kuzingatia kanuni na maadili ya utumishi wa Umma.

"Mkurugenzi karibu sana Arusha DC, watumishi wako tayari kushirikiana nawe, kama ilivyokuwa kwa wakurugenzi waliotanguli, nikuahidi kufanyakazi kwa bidii kama timu ikiwa ni moja ya core value za halmashauri yetu, ambayo iko moyoni kwa watumishi wote"

 Mkurugenzi Mtambule ni Mchumi kitaaluma, akiwa ni mkurugenzi wa nne, tangu kuanzishwa kwa halmashauri ya Arusha mwaka 2007, akiwa ameteuliwa na mheshimiwa Rais kutoka Jiji la Mbeya alikotumika kama Afisa Mipango wa Jiji.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.