Na Elinipa Lupembe
# Amewapongeza wajumbe wote wa Baraza kwa ushirikiano mkubwa wa kusukuma gurudumu la maendeleo katika kuijenga halmashauri, kwa pamoja mmeweza kuisimamia halmashauri na kupata hati safi, kufuatia hoja za CAG za mwaka wa fedha 2021/202, endeleeni kushirikiana na watalaam wa sekta zote ili tuendelee kupata hati safi.
#Maendeleo ya halmashauri yetu, yanategemea maamuzi ya mkutano wa Baraza la Madiwani, kila Diwani ana wajibu wakupitisha maazimio kwa mujibu wa sheria, katika maamuzi ni muhimu kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
#Ili mipango na maazimio mnayoyapanga na kupitisha kwenye vikao vyenu, iweze kutekelezeka, suala la ukusanyaji na usimamizi wa mapato ni jukumu lenu kubwa, shirikianeni na watalamu kuhakikisha mapato yanakusanywa na kutumika kwa kuzingatia taratibu za matumizi ya fedha za Umma.
#Serikali inawategemea sana, waheshimiwa madiwani kuweka mipango ya maendeleo, katika kusimia utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo katika maeneo yenu, hakikisheni kila mtu anashiriki katika usimamizi wa miradi pamoja na kuwashirikisha wananchi wenu kutambua miradi hiyo ni mali yao.
#Serikali inaleta fedha nyingi za miradi kwenye maeneo yenu katika sekata ya afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara, mnalo jukumu la kufuatilia hatua zote za utekelezaji wa miradi hiyo bila kuathiri kanuni na taratibu na kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora unaoendanan na thamani ya fedha.
# Madiwani ndio Wasimamizi wa utekelzaji wa Ilani ya chama kilichopo madarakani, hakikisheni mnaisimamia vema, fedha za miradi yote kwenye maeneo yenu, tunaomba msimamie miradi hiyo kwa uhakika ili iwe na ubora na ikamilike kwa kuzingatia vigezo.
# Wahimizeni watendaji wa kata na vijiji, kufanya mikutano ya vijiji pamoja na kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa kila robo ya mwaka, hakikisheni mnawabana kuleta taarifa kwenye vikao vya WDC, kuna changamoto ya usomaji wa mapato na matumizi, jambo hili linaendelea kupunguza imani ya wanachi kwa serikali yao.
#Simamieni utatuzi wa migogoro katika maeneo yenu kwa kutatua kero za wananchi wanaohangaika katika kupata haki zao, simamieni mamalaka zilizo chini yetu zinazotakiwa kusimamia haki za wananchi na kuhakikisha wanapata haki zao bila upendeleo.
#Madiwani tengeni muda ya kusikiliza kero za wananchi, wananchi waliwachagua kwa kura wakiamini mnakwenda kuwasaidia kutatua na kuondoa kero zao.
#Mimi na kamati yangu ya Ulinzi na Usalama, tumejipambanua kupigania haki za wananchi, maandiko yanasema haki huinua Taifa, tukiwaondolea kero watajikita kwenye shughuli za uzalishaji.
# Masiwani simamieni upatikanaji wa chakula shuleni, tungeni sheria ndogo kwenye maeneo yenu, ili kuwabana na kuhakikisha kila mzazo anapelekwka chakula cha mtoto wake shuleni, toeni elimu kwa wazazi watambue umuhimu wa lishe kwa watoto, oneni umuhimi wa lishe bora kwa watoto, ambayo inanafasi ya ufaulu katika masomo na kuwezakutimiza ndoto zao.
#Suala la ukatili wa kijinsia kwa watoto, ni changamoyo katika maeneo yetu, sisi ni viongzoi hakikisheni watoto wanalindwa na kusimamiwa haki zao, malezi ya watoto hawa ni jukumu letu viongozi, kwa manufaa ya Taifa letu.
# Mnalo jukumu la kusimamia utunzaji wa mazingira katika maeneo yetu, mmeshuhudia madhara yaliyotokana na mvua, yote yamesababishwa na sisi wenyewe, watu wamelima kwenye vyanzo vya maji, kwenye miinuko na kuondoa makinga maji, kila kiongozi akisimama kqenye nafasi yake kwa kuzingatia sheria za mazingira, hatutapata madhara makubwa kiasi hiki.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.