Na Elinipa Lupembe.
Jumla ya Wanafunzi 851 wavulana 395 na wasichana 458, halmashauri ya Arusha wanategemea kufanya mtihani kwa Taifa wa kuhitimu Kidato cha 6 unaonza tarehe 02, Mei 2023 kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amebainisha kuwa mtihani huo wa Taifa unajumuisha watahiniwa wa kidato cha sita na vyuo vya ualimu.
Ameeleza kuwa, tayari maandalizi yote yamefanyika kwa mujibu wa taratibu za Mitihani ya Taifa huku wanafunzi na walimu wasimamizi wameshapewa mafunzo ya usimamizi wa mtihani huo.
Aidha amewataka wasimamizi wa mitihani, kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu wakati wote wa mitihani na kutokujiingiza kwenye aina yoyote ya vitendo vya udanganyifu kwa kuwa, lengo la mitihani hiyo ni kuwapima wanafunzi kulingana na kile walichojifunza kwa miaka yote 2.
"Niwatake watalamu wote wanaohusika na usimamizi wa mitihani, kujiepusha na vitendo vyoyote vya udanganyifu ambavyo ni kinyume na maadili ya mitihani, hakikisheni mnawasimamia wanafunzi hao kwa uaminifu ili waweze kufikia ndoto zao na sio kuwaingiza kwenye matatizo yasiyo ya lazima". Amesisitiza Mkurugenzi Msumi
Hata hivyo Mkuu wa shule ya sekondari Mringa, Mwl. Salim Magaka, amesema kuwa walimu wamewaandaa wanafunzi vema kisaikolojia, kiakili na kimwili, wamejengewa uwezo wa kujiamini wakati wote wa mitihani kwa kuwa mtihani huo ni sawa na mitihani mingine ambayo huifanya mara kwa mara.
"Tuna jumla ya wanafunzi 188, tumewafundisha vizuri kwa kukamilisha mada zote, tumewapa majaribio na mitihani ya kutosha, tumewaandaa kisaikolojia kwa kuwaondoa 'stress' pia, kazi iliyobaki ni kwao, lakini zaidi tunaamini wanafunzi wa shule yetu wataendelea kupata alama A kwa masomo yote" Amebainisha Mkuu huyo wa shule.
Awali Mkuu wa Idara ya Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha, Mwl. Menard Lupenza amefafanua kuwa kati ya watahiniwa 851 wanafanya mitihani wa Kidato cha Sita na watahiniwa 8 wanafanya mtihani wa Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada kwenye vyuo viwili vya Ualimu.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.