Wajumbe wa Kamati ya Siasa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Arumeru, wameanza ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo halmashauri ya Arusha.
Kamati hiyo ya Siasa imeongozwa na Mwenyekiti wa CCM wiliaya ya Arumeru Ndugu Noel Severe wanategemea kukagua jumla ya mira 12 katika sekta Afya, Elimu, Biashara na Uwekezaji na wameanza kwa kutembelea mradi wa Mitambo ya halmashauri.
Miradi itakayotembelewa ni mradi wa Kituo cha Redio, enEnaboishu Fm Redio, Mitambo, Kituo cha Afya Matevesi, Zahanati ya Kijiji cha Lemuguru, Nyumba ya mwalimu shule ya msingi Olemedeye, Shule ya Mchepuo wa Kiingereza Enyorata, Ujenzi vymba vya madarasa na ukamilishaji wa Maabara ya Sayansi shule ya Sekondari Olimitu pamoja na mradi wa Kiwanda cha Matofali Mlangarini.
Ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.