• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI ARUSHA DC, WATAKIWA KUSIMAMIA MASUALA YA LISHE KATIKA MAENEO YAO - DC ARUMERU

Posted on: April 1st, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuzingatia mkakati wa Serikali juu ya masuala ya Lishe bora ya wananchi katika maeneo yao, kupitia mkataba wa Lishe waliosaini,  lengo likiwa kuondoa hali ya udumavu katika jamii na kuwa na jamii yenye afya bora.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, wakati akifungua kikao kazi cha mkatati wa Lishe, kilichojumuisha Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, halmashauri ya Arusha, chenye lengo la kufanya tathmini ya hali ya lishe kwa miaka mitano iliyopita na kusaini mkataba wa mkakati wa Lishe kwa miaka mitano ijayo, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Mhandisi Ruyango, amewaagiza watendaji hao, kuwa na mkakati shirikishi, utakaowashirikisha wananchi, Wahudumu wa Afya, wahudumu wa Afya ngazi ya jamii pamoja na wadau wa maendeleo, kutoa elimu ya Lishe kwa jamii, ili kuhakikisha wananchi wote wanapata ufahamu juu ya lishe bora, hususani kwa wajawazito na watoto.

"Ninawagiza watendaji wote, Lishe iwe agenda ya kudumu katika vikao vyenu vyote kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata pamoja na menejimenti kwa kuwashirikisha waheshimiwa Madiwani, lengo likiwa kuondoa udumavu wa mwili na akili kwa wananchi wote maeneo yotu, kupitia tathmini ya miaka mitano iliyopita, tunatakiwa kufanya vizuri zaidi kwa miaka mitano ijayo" amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewasisitiza Watendaji hao, kuhakikisha kina mama Wajawazito katika maeneo yao wanapata Lishe bora katika siku 1000 za ujauzito, lishe ambayo tafiti zinaonesha ndio inawezesha mtoto aliye tumboni kujenga afya bora ya ubongo na mwili, afya ambayo ndio inategemewa na jamii na Taifa hapo baadaye na kuwasisitiza kutumia vyakula kutoka makundi matano ya vyakula, vyakua ambavyo vinapatikana katika maeneo yote ya Arumeru.

Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amewataka Maafisa watendaji hao, kuhakikisha wajawazito wote katika maeneo yao wanahudhuria kliniki pindi wanapopata ujauzito, wazazi wote wenye watoto wa umri chini ya miaka mitano kuwapeleka watoto hao kliniki, pamoja na kupiga vita tabia ya kina mama wajawazito kujifungulia nyumbani sambamba na kuweka sheria ndogo za kuwashughulikia wale watakaokiuka.

"Ninawasisitiza Maafisa Watendaji wote wa kata na vijiji kufanya kazi kwa kushirikiana kama timu, ili kuhakikisha wananchi wenu wanakula vyakula kwa kuzingatia makundi yatakayowapa lishe bora, wananchi wakiwa na afya bora nguvu kazi itaongezeka na wananchi wakiwa na nguvu, wataleta maendeleo katika maeneo yetu" ameweka wazi Mkurugenzi Msumi.

Afisa Mtendaji Kata ya Ilboru, Wema Sikoi, amekiri kupata uelewa mkubwa juu ya masuala ya Lishe, na kuahidi kwenda kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na serikali kulingana na mkataba waliousani, na kuongeza kuwa, wataongeza kasi ya kuhakikisha wajawazito wanahudhuria kiliniki na wenza wao, pamoja na kuwapatia lishe bora katika siku 1000 za ujauzito, siku ambazo zinaonekana kuwa ni msingi wa afya ya binadamu yoyote.

Hata hivyo Afisa Lishe, Halmasahuri ya Arusha, Doto Milembe, ameyataja makundi ya vyakula yanayopaswa kuliwa ili mtu kuwa na lishe bora ni vyakula vya nafaka na mizizi, vyakula vya nyama na mikunde, mbogamboga na matunda pamoja na sukari na asali na kubainisha kuwa vyakula vyote hivyo vinapatika katika maeneo mengi ya halmashauri ya Arusha.

Awali serikali imeandaa mpango wa Lishe wa miaka mitano 2022 -2027, unaotaka kila mwananchi kuwa kupata lishe bora kwa kula mlo wenye makundi matano ya vyakula kuanzia siku 1000 za mama mjazito, mtoto anapozaliwa mpaka miaka mitano na jamii nzima, mkakati unaoelekeza kuwasainisha mikataba Maafisa Watendaji wa Kata ili kusimamia mkakati huo wa Lishe.

ARUSHA DC

KaziInaendelea✍✍


Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, halmashuri ya Arusha wakati akifungua Kikao kazi cha tathmini ya Lishe kwa miaka mitano na kuweka mikakati ya miaka mitano ijayo, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.


Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, halmashuri ya Arusha wakati wa Kikao kazi cha tathmini ya Lishe kwa miaka mitano na kuweka mikakati ya miaka mitano ijayo, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.


Afisa Mtendaji Kata ya Kiutu, Twati Sukurieti akiweka saini mkataba wa kisimamia masuala ua Lishe katika kata yake kwa kipindi cha miaka mitano,  wakati wa Kikao kazi cha tathmini ya Lishe kwa miaka mitano mikakati ya miaka mitano ijayo, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.


Afisa Lishe halmashauri ya Arusha, Doto Milembe, akitoa tathmini ya hali ya Lishe ya halmashauri ya Arusha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na mikakati ya miaka mitano ijayo, wakati wa  Kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

 

Maafisa Watendaji wa kata na Vijiji  wakisaini mikataba ya Lishe yenye mikakati ya Lishe katika maeneo yao kwa  kipindi cha miaka mitano ijayo, wakati wa  Kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.