• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MHE.MCHENGERWA AONYA VIKUNDI HEWA MIKOPO YA 10%

Posted on: February 9th, 2025

MHE.MCHENGERWA AONYA VIKUNDI HEWA MIKOPO YA 10%


OR-TAMISEMI


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , Mhe.Mohamed Mchengerwa amesema Mkuu wa Mkoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa watakaobainika maeneo yao kuwa na vikundi hewa kwenye mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu watawajibishwa.

Aidha, zaidi ya Sh.Bilioni 234 zinakusudiwa kupelekwa kwa wananchi kwa njia mbili za utoaji mikopo hiyo ambazo ni kupitia Benki kwa Halmashauri 10 na mikopo iliyoboreshwa kwenye Halmashauri 174.


Akizungumza Februari 7, 2025 jijini Dodoma kwenye hafla ya utiaji saini mikataba kati ya Halmashauri 10 na Benki tatu ya utoaji mikopo hiyo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani, Mhe. Mchengerwa amesema kila mmoja afuatilie fedha hizo kuhakikisha zikishuka kama ilivyokusudiwa kwa walengwa ili zitabadili maisha yao.


Amesisitiza uadilifu wa kwenye fedha hizo na kufuatilia kwa kina vikundi vyote na kuvijua na asisikie vikundi hewa.


“Fedha hizi ni za moto wajibu wetu ni kumsaidia Rais fedha hizi zisiende kuchezewa, naelekeza kikundi hewa kitakachobainika eneo lolote viongozi wa eneo hilo mtapaswa kuwajibika, tumieni vyombo mnavyosimamia kwenye mikoa na wilaya kuhakikisha hakuna vikundi hewa, fedha zisimamiwe na kurejeshwa.”

“Nazielekeza Mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kuchangia fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo hii kwa mujibu wa sheria ya fedha za serikali za mitaa, na Katibu Mkuu niletee orodha kama kuna halmashauri ambazo hazijachangia na zinadorora kuchangia na kama kuna halmashauri ambayo haijatekeleza maelekezo ya Rais,”amesema.


Amesema Benki ya NMB itafanya kazi kwenye halmashauri za wilaya za Bumbuli, Itilima, Newala, Manispaa ya Songea, Jiji la Dodoma na Jiji la Dar es salaam huku benki ya CRDB itafanya kazi Wilaya za Nkasi, Mji wa Mbulu, Manispaa ya Kigoma, Jiji la Dodoma na Jiji la Dar es salaam na Benki ya Biashara ya Uchumi itafanya kazi Halmashauri ya Wilaya ya Siha.


Awali, Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Adolf Ndunguru amesema kusainiwa mikataba hiyo ni mwanzo wa mapinduzi ya kuhakikisha mikopo hiyo ya asilimia 10 inakuwa na tija tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.