• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MILIONI 200 ZAKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA 4 ZA WATUMISHI WA AFYA KWENYE KATA TATU.

Posted on: November 25th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Katika kutekelazaji wa mikakati ya serikali ya kuboresha miundo mbinu kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya, serikali imefanikiwa kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za watumishi lengo likiwani kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya katika maeneo yao na kwa muda wote.

Katika mwaka wa fedha 2021/2022, halmashauri ya Arusha ilipokea kiasi cha shilingi milioni 200 fedha kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 4 za watumishi kwenye vituo 4 vya Afya vilivyopo maeneo ya pembezoni.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amebainisha kuwa kiasi hicho cha fedha kimetumika kujenga nyumba 4 za watumishi wa afya kwa gharama ya shilingi milioni 50 kwa kila nyumba.

"Fedha hizo zimejenga nyumba za watumishi kwenye maeneo ambayo watumishi hawakuwa na mahali pa kuishi na kulazimika kuishi mbali na vituo vyao vya kazi, nyumba hizi zimejengwa kwenye zahanati za LoovLukuny na Ilkerini kata ya Kisongo, zahanati ya  Ilkirevi kata ya Oltoroto,  na kituo cha Afya Nduruma".Amefafanua Mkurugenzi Msumi

Naye Mkuu wa Idara ya Mipango, Anna Urio, amesema kuwa fedha hizo ni utekelezaji wa malengo ya bajeti ya halmashauri ya mwaka wa fedha 2021/2022  ulioishia June 2022 wa kuboresha mazingira ya watumishi ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi.

Naye Mganga Mfawidhi zahanati ya Ilkirevi kata ya Olturoto,  Atu Sanga, amsema kuwa uwepo wa nyumba ya mtumishi wa afya, utaongeza tija na ufanisi wa kazi, ikiwa nipamoja na kutoa huduma za afya kwa masaa 24.

"Mtumishi akiishi eneo la kazi inampunguzia gharama za kulipa kodi ya nyumba lakini inatuwezesha kutoa hudma za emergence hasa nyakati za usiku, wagonjwa wanakuwa na uhakika wa kupata matibabu". Amefafanua  Mganga huyo Mfawaidhi.

Hata hivyo Diwani wa kata ya Olturoto, ameishukuru seikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimwa Samia Suluhu Hassan, kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM,  katika sekta zote hususani sekta ya afya, sekta ambayo ni muhimu kwa afya za wananchi.

"Ninampongeza na kumshukuru mheshimiwa Rais, kwa niaba ya wananchi wa Olturoto, ujenzi wa nyumba ya mtumishi  ni wazi utaongeza tija katika utendaji wa kazi lakini uwanda mpana wa upatikanaji na utoaji wa huduma za afya kwa wananchi sambamba na kupunguza vifo vya wanawake na watoto" Amesisitiza Mhe. Simon

Ujenzi wa miundombinu ya afya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 -2025 wa kuongezeka vituo kutolea huduma za afya nchini ikiwemo zahanati, vituo vya afya na hospitali pamoja na nyumba za wahudumu wa afya.


ARUSHA DC

KaziInaendelea ✍✍✍


PICHA ZA MAJENGO YA NYUMBA ZA WATUMISHI

Muonekano wa Nyumba ya Mtumishi Kituo chaAfya Nduruma kata ya Nduruma

Muonekano wa Nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Loovilukuny kata ya Kisongo

Muonekano wa Nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Ilkerini  kata ya Kisongo

Muonekano wa Nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Ilkerini  kata ya Kisongo

Muonekano wa Nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Ilkirevi kata ya Olturoto

Muonekano wa Nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Ilkirevi kata ya Olturoto





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.