Na. Elinipa Lupembe.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na utekelezaji wa miradi ya Mpango wa Elimu Lipa Kutokana na Matokeo 'EP4R', imetoa kiasi cha shilingi milioni 670.8 kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu ya shule za msingi na sekondari, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
Akizungumza ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule amethibitisha kupokea fedha hizo kutoka serikalini, fedha ambazo zinatumika kujenga miundombinu ya shule 7 za msingi na shule 3 sekondari, miradi ambayo utekelezaji wake uko kwenye hatua za awali za ujenzi.
Mkurugenzi huyo ameweka wazi mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo, kuwa, shilingi milioni 38 zitajenga vyumba 19 vya madarasa, shilingi milioni 100 kujenga nyumba 2 za walimu zenye sehemu 2 (2 in 1), shilingi milioni 80 kujenga bweni la wanafunzi na shilingi milioni 26.8 fedha za kujenga vyoo vinne vyenye matundu 23.
"Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa jumla ya vyumba 19 vya madarasa na matumdu 23 ya vyoo, ikiwa vyumba 12 vya madarasa na matundu 18 ya vyoo kwa shule 7 za msingi, na vyumba 7 vya madarasa kwa shule 3 za sekondari huku ujenzi wa matundu 5 ya choo yakijengwa kwenye shule mpya ya sekondari ya sekondari Losinoni pekee" ameainisha Mkurugenzi huyo.
Naye Afisa Elimu Sekondari halmashauri ya Arusha, Menard Lupenza, amekiri ujio wa fedha za ujenzi wa miundombinu ya shule, umekuja wakati muafaka, kwa kuwa bado shule nyingi zinamahitaji ya miundombinu ya madarasa na vyoo, mabweni na nyumba za walimu, uhitaji unaotokana na ongeezeko kubwa la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule za sekondari kwa sasa.
Ameongeza kuwa licha ya kuwa uhitaji huo upo kwenye shule nyingi lakini upo zaidi kwenye shule mpya za sekondari, zilizoanzishwa na kusajiliwa mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo shule ya sekondari Losinoni kata ya Oldoonyowas, imefanikiwa kupata fedha za kujenga vyumba vitatu vya madarasa, nyumba mbili za walimu zenye sehemu mbili (2 in 1) na choo cha wanafunzi chenye matundu matano.
" Kiasi hicho cha fedha, kimehusisha ujenzi wa miundombinu kwenye shule mpya ya Sekondari Lesinoni, shule ambayo bado ni changa na bado inamahitaji makubwa ya miundombinu, utekelwzaji wa miradi hiyo, itaongeza tija na ufanisi kwa maendeleo ya shule na wanafunzi wa maeneo ya kata ya Oldonyowas". Amesema Afisa elimu huyo.
Naye Kaimu Mhandisi wa Ujenzi, mhandisi Bibie Manzi, amesema kuwa ujenzi wa miradi hiyo yote, itatekelezwa kwa kutumia wakandarasi wa maeneo husika 'forced account', na tayari utekelezaji wa miradi hiyo uko kwenye hatua za awali na miradi yote inategemea kukamilika mwishoshoni mwa mwezi Oktoba.
PICHA ZA HATUA ZA AWALI ZA UJENZI WA MIUNDOMBINU HIYO
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.