• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MILIONI 90 ZA TOZO ZAJENGA NYUMBA YA WATUMISHI KITUO CHA AFYA MWANDET

Posted on: May 31st, 2022

Na Elinipa Lupembe.

Serikali kupitia wizara ya Afya, inaendelea na mkakati wa kuboresha miundombinu ya huduma za afya, unaoenda sambamba na ujenzi wa nyumba za watumishi wa Afya, ili wahudumu kuwa na makzi katika maeneo yao ya kazi pamoja na kuhakikisha wananchi hasa wa maeneo ya pembezoni wanapata huduma za afya kwa masaa 24.

Kupitia mkakati huo, wakazi wa kata ya Mwandeti na vitongoji vyake wamepata neema hiyo, ya kuongezewa miundombinu katika, iliyokuwa zahanati ya Mwandeti na kuwa kituo cha afya, sambamba na ujenzi wa nyumba ya wahudumu wa afya.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi ameweka wazi kuwa, halmashauri yake, ilipokea kiasi cha shilingi milioni 90, kutoka serikali kuu, ikiwa ni fedha za tozo za miamala ya simu, kwa ajili kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa kituo kipya cha afya Mwandeti, yenye sehemu ya kuishi watumishi watatu (3 in 1).

Aidha amefafanua kuwa, utekelezaji wa mradi huo, unaendelea vizuri, uko hatua za ukamilishaji, na unategemea kukamilika mwishoni mwa mwaka huu wa fedha, tayari kwa watumishi wa kituo hicho cha afya, kuanza kuishi na kuendelea na majukumu yao ya kuwahudumia wagonjwa, kama malengo ya serilali yanavyoainisha.

"Niseme tu, serikali ya awamu ya sita inatambua, kazi kubwa inayofanywa na wahudumu wa afya, inatambua mazingira yao ya kazi, ndio maana ina mkakati wa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya, pamoja na mazingira rafiki ya kuishi watumishi wa afya, hususan maneo ya pembezoni, ameneo ambayo yanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nyumba za kuishi" amefafanua Mkurugenzi Msumi.

Naye Mganga Mfawidhi Zahanati ya Mwandeti, Dkt. Aidan Martin amesema kuwa, ujenzi wa nyumba hizo za watumishi, umekuja kwa wakati sahihi kwa kuwa, uwepo wa nyumba za watumishi katika eneo la kazi, utawaongezea ari ya kufanya kazi, itaongeza weledi katika kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na  utoaji na upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa kwa urahisi na kwa haraka wa muda wote wa siku.

"Daktari na wauguzi wanaposihi ndani ya eneo  la kazi, inawarahisishia utekelezaji wa majukumu yao ya kazi, kuingia kazini kwa wakati, kutoa huduma kwa haraka hususani huduma za 'emergence' hasa wakati wa usiku, lakini pia inaongeza wigo kwa wagonjwa kupata huduma kwa saa 24, kwa kuwa wauguzi wanapatikana eneo hilo kwa muda wote" amesema Dkt. Martin 

Awali ujenzi wa nyumba hiyo ya watumsihi wa afya, umeenda samabamba na upanuzi wa miundombinu ya zahanati ya Mwandeti ili kuwa kituo cha afya, upanuzi uliohusisha ujenzi wa nyumba hiyo ya watumishi, jengo la wagonjwa wa nje, jengo la mama na mtoto, maabara, jengo la  X-ray na Laundry kwa gharama ya shilingi milioni 500.

ARUSHA DC Kaziinaendelea✍✍

#mamaanaupigamwaingi#

#Kaziinaendelea#

Maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya watumishi wa afya, kituo cha afya Mwandeti, yenye uwezo wa kuishi familia tatu (3in 1) inajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 90, fedha za Tozo za miamala ya simu.








Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.