Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Ndugu Seleman H. Msumi, ameungana na wananchi na wadau mbalimbali kushiriki Msimu wa Tatu wa Mbio za Msituni (Meru Forest Adventure Race) zilizofanyika katika maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Meru USA
Katika mashindano hayo yaliyojumuisha wakimbiaji wa umbali wa kilometa 5, 10 na 20, Ndugu Msumi alikimbia kilomita 10 kupitia njia za asili ndani ya Msitu wa Meru, akionesha mfano wa kuhamasisha wananchi kushiriki katika michezo na kulinda na kutunza Mazingira.

Akizungumza baada ya kumaliza mbio, Mkurugenzi Mtendaji alisisitiza umuhimu wa michezo kama nyenzo ya kujenga afya, mshikamano wa kijamii na pia kuhamasisha utunzaji wa misitu na vyanzo vya maji.
“Mbio hizi si za ushindani pekee, bali ni fursa ya kuutangaza, kuhamasisha utalii wa ndani, na kuwahimiza wananchi kutunza rasilimali za asili zinazotuzunguka,” alisema Msumi.
Mashindano hayo ya Meru Forest Adventure Race yameendelea kujipatia umaarufu kila mwaka, yakivutia washiriki kutoka sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi, huku yakiwa chachu ya kukuza michezo, utalii na utunzaji wa mazingira.


Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.