Na Elinipa Lupembe
Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Kujadili taarifa za Kata kwa Kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 cha kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2023 umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha, huku
Waheshimiwa Madiwani wakiipongeza serikali ya awamu ya sita k wa kuendelea kuboresha huduma za jamii kwenye Kata zao na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi.
Mkutano huo, waheshimiwa Madiwani wa kata zote 27 wanawasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maendeleo za Kata zao kwa kipindi cha robo ya nne na ya mwisho kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Hata hivyo waheshimiwa Madiwani wameishukuru serikali kwa fedha nyingi za miradi kisekta, fedha ambazo zinatekeleza miradi inayokwenda kutatua changamoto nyingi za wananchi hasa waishio vijijini.
Aidha Waheshimiwa Madiwani hao, wameelezea kuwa licha ya mafanikio hayo bado wanakabiliwa na changamoto za miundombinu mibovu ya barabara katika maeneo mengi, maji pamoja na ukosefu wa umeme wa REA kwa baadhi ya vitongoji kwenye baadhi ya vijiji na kuiomba serikali kuweka mipango ya kutatua kero hizo kwa manufaa ya wananchi wao.
Mkutano huo umefanyika kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za Kata, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.