Mapema leo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Mwinyi Ahmed Mwinyi, amefanya kikao kazi na wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma zinazotoa huduma kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Kikao hicho kililenga kujadili namna ya kuongeza wigo na ufanisi wa utoaji huduma, sambamba na kuimarisha mshikamano baina ya taasisi hizo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, kwa wakati na kwa uwazi.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mwinyi aliwataka viongozi wa taasisi hizo kushirikiana kwa karibu zaidi, kuondoa urasimu usio wa lazima na kuweka mkakati wa pamoja wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Serikali na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Baada ya kikao, viongozi walipata fursa ya kujadiliana kwa undani kuhusu mikakati ya utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa, huku wakiahidi kuongeza bidii katika majukumu yao ya kila siku.
Matukio ya picha mara baada ya kikao yameonesha mshikamano na mshikamo wa pamoja wa viongozi hao katika kuhakikisha maendeleo ya Wilaya ya Arumeru yanapiga hatua kubwa


Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.