Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Mwinyi A. Mwinyi, leo tarehe 31 Agosti 2025, amezindua rasmi mashindano ya Meru Forest Adventure Race msimu wa tatu katika viwanja vya Meru Forest. Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa michezo, pamoja na wakazi wa eneo hilo waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kipekee linalolenga kukuza utalii wa ndani na michezo ya kijamii.
Mashindano hayo ya Adventure Race yametoa fursa kwa vijana na washiriki mbalimbali waliooneshasha vipaji vyao katika michezo ya mbio, baiskeli na shughuli za mazoezi ya msituni.
Aidha, yamekusudiwa pia kuhamasisha uhifadhi wa mazingira ya msitu wa Meru na kukuza mshikamano wa kijamii kupitia michezo.



Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.