Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Mwinyi Ahmed Mwinyi, amehitimisha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria 2025 katika kikosi cha 833 KJ Oljoro chini ya Operesheni Nishati Safi.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mheshimiwa Mwinyi aliwataka vijana hao kuendelea kuishi kwa kuzingatia viapo vyao, kuwa raia wenye nidhamu, pamoja na kushirikiana katika kulinda na kujenga taifa. Alisisitiza kuwa mafunzo ya JKT si tu yanawajengea uzalendo na mshikamano, bali pia yanawapa ujuzi na maadili muhimu kwa maisha ya kila siku.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya aliwahimiza vijana kuwa mabalozi wazuri wa taifa lao popote watakapokuwa, kwa kutenda mema, kushirikiana na jamii, na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kudhoofisha heshima na mshikamano wa taifa. Alimalizia kwa kuipongeza JKT kwa kazi kubwa ya malezi na ujenzi wa vijana wa Kitanzania.




Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.