• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mwanamke wa kwanza kufanyiwa upasuaji kituo cha afya Nduruma atoa ushuhuda kwa Katibu Mkuu OR-TAMISEMI

Posted on: September 16th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Mwanamke wa kwanza kufanyiwa upasuaji, kwenye kituo cha Afya Nduruma, mara baada ya kituo hicho kujengwa majengo mapya ikiwemo jengo la upasuaji, ametoa ushuhuda wa furaha aliyonayo, mbele ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandusi Joseph Mwamhanga, wakati wa ziara yake ya kikazi ndani ya halmashauri ya Arusha.

Mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Maria Seleman, amesema kuwa, wakati wa ujauzito wake alipanga kujifungulia kwenye  kituo hicho cha afya, mara baada ya serikali kujenga kuboresha miundo mbinu ya kituo hicho, na awali hakufahamu kuwa angetakiwa kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Baada ya kufikishwa katika kituo hicho cha afya na kufanyiwa uchunguzi na madaktari, walishauri  kufanyiwa upasuaji na kumfanya kuwa mgonjwa wa kwanza kutumia jengo hilo jipya la upasuaji, huku akiwashukuru wahudumu wa afya kwa huduma bora waliompatia, mpaka sasa wanaendelea vizuri yeye na mtoto wake wakiwa wenye nguvu na afya bora.

Hata hivyo, katibu mkuu huyo, a mefurahishwa na ushuhuda wa mama huyo, aliyepata huduma ya upasuaji katika kituo hicho cha afya na kusisitiza kuwa hilo ndio lengo la Serikali ya awamu ya tano, la kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua kwa kujenga vituo vya afya na kuboresha huduma hizo, ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ndani ya maeneo yao bila kutembea umbali mrefu.

Aidha amewataka wananchi wa eneo hilo kuthamini gharama zilizotumika kuwekeza kwenye majengo na vifaa tiba, na kufahamu kuwa kituo hicho ni mali yao na kuwahimiza kukitunza na kukilinda, huku akiwataka wauguzi na madaktari kutoahuduma stahiki kwa wagonjwa bila ubaguzi.

Aidha Katibu mkuu, ameahidi kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mionzi 'X-ray' katika kituo hicho, kwa kuwa tayari serikali imeshaleta vifaa vya mionzi, na kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri, kufanza makisio ya gharama za ujenzi wa jengo hilo.

"Kwa kuwa tayari vifaa vya x-ray vimeshafika, niahidi kutafuta fedha za kujenga jengo la mionzi kwa haraka ili vifaa hivyo vianze kutumika na wananchi wapate huduma zote kituoni hapo" amesema Katibu mkuu huyo.

Naye mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, licha ya kuishukuru na kuipongeza serikali ya Rais Magufuli, ameahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya wilaya yake, kwa kuhakikisga wananchi wanapata huma bora kwa sekta zote, kama mikakati ya serikali inavyoelekeza.

Akisoma taarifa ya kituo hicho, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Nduruma Dkt. Joseph Ideva, amesema kuwa serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, maabara, jengo la kuhifadhia maiti, kichomea taka, nyumba ya mganga, pamoja na kuleta vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 327 ambapo majengo yote yamekamilika na tayari wananchi wameanza kupata huduma.
Ameongeza kuwampaka sasa upatikanaji wa dawa za msingi, katika kituo hicho ni wa zaidi ya asilimia 95, na kuwataka wananchi kufika kituoni hapo kupata huduma za afya na kuachana na dhana potofu za kwenda kwenye hospitali za binafsi.  


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.