Na Elinipa Lupembe
Mwenyekiti halmashauri ya Arusha Mhe. Ojung'u Piniel Salekwa akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani la robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba mpaka Desemba 2022.
Mheshimiwa Mwenyekiti licha ya kuwakaribisha wajumbe kwenye mkutano huo amewataka kushiriki kwa pamoja kutoa mawazo, maoni na ushauri kwa uhuru, ukweli na uwazi kwa kujikita zaidi kwenye Agenda 10 za mkutano, kwa ajili ya maslahi mapana ya halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mheshimiwa Ojung'u amebainisha kuwa mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za Serikali za Mitaa na uendeshaji wa Halmashauri, ukiwa na Agenda 10 huku Agenda kuu zikiwa ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo, taarifa ya Mapato na Matumizi ya mwezi Desemba 2022, Taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya robo ya pili za Halmashauri, Wakala wa Barbara Mijini na Vijijini (TARURA), Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Wakala wa Umeme Vijijini (REA), pamoja na Kupitisha Mihtasari ya Vikao vya robo vya Kamati za nne za Kudumu.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziInaendelea✍✍✍
PICHA ZA MATUKIO MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.