• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

NGO's ARUSHA DC ZAWASILISHA TAARIFA ZA ROBO YA NNE YA MWAKA WA 2022.

Posted on: February 1st, 2023

Na Elinipa Lupembe.

Jumla ya mashirika yasiyo ya kiserikali 30 kati ya 46 ya yanayofanyakazi ndani ya mipaka ya halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, yamewasilisha taarifa za robo ya nne kwa mwaka 2022, huku mashirika hayo yakisisitizwa kuelimisha jamii juu ya ulawiti kwa watoto wa kiume.

Mashirika hayo yamewasilisha taarifa zao zilizoainisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizofanywa na mashirika hayo kwa kipindi cha robo hiyo ya nne na ya mwisho kwa mwaka 2022,  kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Arusha.

Katika kikao hicho kila mwakilishi wa shirika alipata wasaa wa kuelezea utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo iliyofanyika kwa kipindi cha robo hiyo huku wakielezea ongezeko la matukio ya ulawiti yanayowakabili watoto wa kiume ndani ya jamii kwa sasa.

"Kama mashirika tunapswa tuone namna ya kuelekeza nguvu za kuhamasisha na kutoa elimu kwa  watoto wa kiume kujitambua na kujilinda dhidi ya ulawiti, huku tukihamasisha jamii kuwalinda watoto wa kiume kama ilivyo kwa watoto wa kike.

Aidha Mashirika hayo yamepongeza utaratibu huo unaofanywa na serikali na kuueleze ni utaratibu unaowakutanisha pamoja na kufahamiana huku kila shirika likifahamu miradi innayofanywa na shirika jingine katika eneo husika.

Amesema kuwa uwepo wa kikao hicho licha ya kufahamiana, unawapa fursa ya kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo namna ya  kutatua changamoto zinazoikabili jamii

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, ameweka wazi kuridhishwa na shughuli zinazofanywa na ASAS hizo katika halmashauri, miradi ambayo inawakwamua wananchi kutoka kwenye hali duni na kwenda hali nzuri.

Ameongeza serikali inatambua na kuthamini kazi zinazofanywa na ASAS za kiraia, kwa kuwa mnaisaidia serikali kutimiza majukumu yake ya kuihudumia jamii.

"Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa mashirika kwa kutambua umuhimu wa huduma mnazozitoa kwa jamii, ni huduma za kiimani zaidi, mngeweza kufanya vinginevyo lakini mmejikita kuwahudumia wananchi hususani wasio na uwezo ili wajikwamue". Amefafanua Msumi.

Naye mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Arusha Stedvant Kileo, ameyataka mashirikia hayo kuona namna ya kuwekeza nguvu katika kuwalinda na kuwajengea uwezo watoto wa kiume dhidi ya  vitendo vya ulawiti, matukio ambayo yameshika kasi katika jamii yetu.

"Niwaombe mashirika katika miradi mnayoifanya, kuingiza agenda ya kupinga na kupambana na matukio ya ulawiti kwa watoto wa kiume, changamoto ambayo inashika kasi kwenye jamii kwa sasa". Amesisitiza Kileo

Kikao hicho kimefanyika kwa mujibu wa sheria za serikali zinayoyataka  mashirika yasiyo ya kiserikali kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli na miradi wanayoifanya kila robo ya mwaka, mwaka unaoanzia mwezi Januari mpaka Desemba.


"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"

#KaziIendelee✍✍











Matangazo

  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022 tarehe 09.05.2022 May 08, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA ARUSHA DC,BW.SELEMAN MSUMI AKIWA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO KATIKA MASDHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA ARUSHA

    May 02, 2025
  • HERI YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • HERI YA SIKU YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • MHE. MAJALIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.